Tanzania Yapiga Hatua Usambazaji wa Maji Vijijini
Tanzania
yapiga hatua katika usambaji wa huduma za upatikanaji wa maji safi na
salama mijini toka asilimia 45 mwaka 2015 hadi 95 mwaka huu na asilimia 46 mwaka 2015 hadi asilimia 65 mwaka huu kwa vijijini.
Hayo
yamebainishwa na Mkrugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na MSEMAJI Mkuu
wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari leo Jijini Dar es Salaam kati mkutano wake wa kawaida wa kila
mwezi kuelezea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na
Serikali.
Akizungumza
katika mkutano huo, Dk. Abbasi amesema kuwa mwaka 2015, Serikali ya
Awamu ya Tano iliweka lengo la kufikisha maji vijijini kwa asilimia 85
na mijini asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.
Dkt
Abbasi amesema kuwa katika kufikia lengo hilo kazi kubwa imefanyika
ambapo zaidi ya miradi 289 na vituo zaidi ya 89,780 vimekamilika ambapo
Serikali imetumia zaidi ya TZS bilioni 336.15.
“Kazi kubwa inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali vijijini ikiwemo kukamilisha vituo 44,590 vya maji.” Alisema Dkt. Abbasi
Hadi
Septemba mwaka huu zaidi ya miradi mikubwa 17 ya maji imekamilishwa
ambapo zimetumika zaidi ya TZS bilioni 823.61. Wakati miradi mingine
mikubwa zaidi ya 35 ya maji ikiendelea kukamilishwa nchini, wastani wa
upatikanaji wa maji safi mijini umefikia asilimia 80.
Kwa
uwekezaji huu, wastani wa jumla wa upatikanaji wa maji vijijini
umepanda kutoka chini ya asilimia 46 mwaka 2015 hadi asilimia 65 mwaka
huu huku kwa upande wa mijini, mwaka 2015 Serikali iliweka lengo la
kufikisha maji kwa asilimia 95 kwa wakazi wa mijini kutoka wastani wa
asilimia 67;
Katika
hatua nyingine Dkt. Abbasi alitumia mkutano huo kuwaondoa hofu wakulima
wa zao la Korosho akisema kuwa kumeanza kuibuka wasiwasi katika jamii
na baadhi ya watu kuanza kuwatisha wakulima kuwa msimu mpya wa korosho
unakuja, watakosa maghala ya kuhifadhi korosho zao.
“Niwahakikishie
wakulima kuwa hadi kufikia Septemba 30, 2019, Serikali imeshauza
korosho zote kwa jumla ya wanunuzi 21 wa ndani na nje ya nchi. Kuna tani
zaidi ya 4,595.90 zitabanguliwa nchini na zaidi ya tani 211, 587 ambapo
tani 107,187 zitapitia Bandari ya Dar na tani 104,400 kupitia Bandari
ya Mtwara zitasafirishwa kwenda nje ya Tanzania,” alisisitiza Dkt.
Abbasi.
Alifafanua
kuwa hadi sasa zaidi ya tani 98,860 zimekwishachukuliwa na kusafirishwa
nje ya nchi kupitia Bandari za Mtwara na Dar sawa na asilimia 41 ya
korosho zote na zoezi la kuondoa korosho iliyobaki kupelekwa kwa
wanunuzi linatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 21 mwaka huu.
“Naomba
kusisitiza tena, faida kubwa ya mchakato huu ni kwa wakulima kupata bei
ya haki katika zao la korosho lakini funzo la korosho si tu limeweka
mazingira mazuri zaidi katika misimu ijayo ambapo korosho itanunuliwa
kwa mfumo madhubuti lakini pia mazao mengine yamepata nguvu ya kuwekewa
mifumo na hivyo wakulima kupata bei inayowanufaisha kwa kuwapa
faida.”Alisema Dkt. Abbasi.
Msemaji
Mkuu wa Serikali amekuwa na utamaduni wa kuzungumza na wananchi kila
mwanzoni mwa mwezi kupitia vyomba vya habari kwa lengo la kuhabarisha
umma juu ya hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John
Pombe Magufuli ili wananchi taarifa sahihi za namna Serikali yao
inavyowajali katika kuwaletea maendeleo.
Post a Comment