Ads

MEYA KUMBILAMOTO AKERWA WANAFUNZI VINGUNGUTI KUNUNULIWA TAULO ZA KIKE NA WANAUME ,ATOA MSAADA BOX 20 KUNUSURU HALI HIYO.



Na John  Luhende
Mwamba wa habari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ametoa msaada wa box 20 za  taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Vingunguti    ikiwa utekelezaji wa mikakati yake ya kuhakikisha Manispaa ya Ilala inapata mafanikio kielimu hasa  watoto wa kike. 

Meya Kumbilamoto  amesema amefikia hatua  ya kugawa taulo za kike  baada ya kubaini kuwa baadhi ya Watoto katika  shule ya Sekondari  Vingunguti wamekuwa wakiingia katika mahusiano  kwasababu ya kununuliwa  taulo hizo.

“Tulikuwa na kikao cha wazazi hapa shuleni mwezi mmoja uliopita  wazai na walimu walizungumza changamoto za watro wakike , Matron akasema kunamtoto alikutwa na taulo zakike kwenye bagi alipomuuliza kazipata wapi akasema alinunuliwa na mwanaume ndipo nikalichukua kama diwani nimeamua kuwasaidia watoto hawa ili wasikatishe masomo yao wakiwa katika hali zao zahatari”Alisema 

Aidha Kumbilamoto amesema  zoezi  hilo litakuwa endelevu na katika  hatua nyingine  katika kukabiliana na upungufu wa madarasa  katika shule hiyo amesema Manispaa ya Ilala imetenga shilingi million 150 kwaajili ya kuongeza madarasa  katika shule hiyo .

Ukosefu wa taulo zake mashuleni kumechangia utoro kwa watoto wa kike kama alivyoeleza  mwalimu wa Malezi  Julietha Sanga
Kwa upande wao wanafunzi wakike shuleni hapo wamemshukuru kumbilamoto kwa msaada huo .

‘’Naitwa Amina Jumanne Kigese  kwaniaba ya wanafunzi wakike namshukuru sana Meya kwa mba ameonyesha namna gani anatuoenda  maana sisi kweli tunakutana na changamoto nyingi katika  mazingira yetu wengi ni masikini ndiyo maana wasichana wamekuwa wakishawishika kujiingiza katika  vitendo vya mapenzi ili wapewe  pedi” Alisema

No comments