Ads

MCHUNGAJI SINDANO AMEZITAKA TAASISI NCHINI KUSAIDIA WATU WENYE UWITAJI.

Mwambawahabari 
Mchungaji Evancy Sindano wa huduma ya Manm Ministry ya Tabata Kisukuru akimkabizi zawadi Afisa Ustawi wa Jamii  Kigamboni Community Center(KCC) Rehema Salika.

Na Maria Kaira, Mwambawahabari
Taasisi mbalimbali hapa nchini zimetakiwa kutoka na kuwasaidia watu wenye uwitaji ili nao wapate furaha nakuona kuwa wanathaminika katika Jamii.

 Hayo yamesemwa na  Mchungaji Evancy Sindano wa huduma ya Manm Ministry iliyopo Tabata Kisukuru wakati wa utoaji msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yatima KCC Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Amesema jamii inatakiwa iguswe kwa kuonesha upendo  kwa kuwatafuta watu wenye uwitaji na kuwasaidia chochote walichojaliwa na Mungu ili nawao wajione sawa na watu wengine.

"Watoto hawa ni viongozi wa baadae,hawajapenda kuishi katika mazingira haya tujitoe kwa moyo mmoja kuwawezesha"amesema

Amesema kipaumbele chao walichojiwekea katika huduma yao ni kuwakumbuka watu wenye uwitaji kila baada ya miezi mitatu ambapo zoezi hilo litakuwa endelevu. 

Aidha Mratibu wa kitengo cha kuwasaidia watoto yatima na wajane wa Manm Minisrty Adelaida Alex amesema zoezi hilo litakuwa endelevu,huku akitoa wito kwa jamii kuwasaidia wale wasio jiweza ili kuwaonesha upendo maana kwa kufanya hivyo ni ibada iliyo njema. 

"Tulikuwa tunaenda hospitali kutoa huduma safari hii tumeona tuwakumbuke watoto yatima na kuwapa faraja"amesema

Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii wa KCC Rehema Salika ameishukuru huduma ya Manm kwa mchongo wao walioutoa katika kituo hicho,kwa kuwakumbuka watu wenye uwitaji kwa kutoa msaada mbalimbali. 
  
Pia ametoa wito kwa Makanisa,Mashirika na watu binafsi kuwakumbuka watoto wanaolelewa kwenye vituo ili nawao wajione wapo nyumbani. 

Mtoto anayeishi kwenye kituo hiko Suleman Mohamed ameipongeza huduma ya Manm kwa kujitoa kwao  kushiriki pamoja nao na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia. 

No comments