MBUNGE JUMAA AMEGAWA BASKELI 125 KWA AJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA
NA HERI SHAABAN(MLANDIZI)
MBUNGE wa Kibaha Vijijni Hamoud Jumaa amegawa baskeli 125 kwa Makatibu Kata wa chama cha Mapinduzi CCM pamoja na makatibu wa Jumuiya za chama kwa ajili ya kuwawezesha kusimamia uchaguzi wa Serikali ya Mtaa Kibaha Vijijini ili CCM ibuke kwa kishindo.
Baskeli hizo zimegaiwa na mgeni rasmi Katibu wa Oganization Taifa Pereira Silima katika kikao cha halmashauri kuu Wilaya Kibaha Vijijini.
Mbunge Jumaa alisema ni sehemu ya utaratibu wake ambao kajiwekea kwa viongozi wa chama wakati wa uchaguzi kuwapa vitendea kazi ili kukiwezesha chama cha mapinduzi ushindi .
"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM itashinda Vijiji vyote 26 na Vitongoji 102 mwaka huu nimewapa baskeli hizi wazitumie kwa ajili ya shughuli za chama zote " alisema Jumaa
Jumaa alisema baskeli hizo alizotoa
125 kwa ajili ya Makatibu wa matawi na makatibu Jumuiya za chama kwa dhumuni la kusaidia shughuli za uchaguzi katika Jimbo la Kibaha Vijijini.
Amewataka baskeli hizo zitumike kwa malengo yaliokusudiwa katika shughuli za CCM.
Amewataka wana ccm na wanachi kukipigia chama cha Mapinduzi ambacho kinatekeleza Ilani kwa vitendo Wachague Wenyeviti wa Serikali za Mitaa watakaoleta chachu ya Maendeleo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Katibu wa Oganization Taifa Pereira Silima alimpongeza Mbunge Jumaa kwa kuwajali wapiganaji wa chama cha Mapinduzi kwa kuwapa baskeli waweze kuzitumia katika kusaka dola.
Pereira aliwataka wana CCM kutunza mali za chama na kuzitumia kwa malengo yaliokusudiwa .
Aliwataka watanzania kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za utekelezaji Ilani kwa vitendo na kusema mazuri ambayo Rais anafanya katika kukuza uchumi wa Tanzania ya viwanda.
Aidha pia aliwataka wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini kushirikiana na mbunge wao katika kukuza Maendele na kumsaidia Rais.
Pereira alisema chama cha Mapinduzi kila siku kinaimalika wana CCM wanatembea kifua mbele na Jimbo la Kibaha Vijijini lipo salama katika sekta zote
Mwisho
Post a Comment