Azam Tv wajitokeza kurusha live pambano Bondia Mwakinyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv Bw. Tido Mhando (kulia) wakipongezana na Promota Jay Msangi (kushoto) baada kutia sahihi ya makubaliano ya kurusha mubashara pambano la kistoria katia bondia mtanzania Hassan Mwakinyo pamoja Mfilipino Arney Tinampay utakaopigwa siku ya Novemba 29 mwaka huu.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kituo cha runinga cha Azam Tv kinatarajia kurusha mubashara pambano la kimataifa kati Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo na mpinzani wake, Arney Tinampay kutoka Ufilipino linalotarajiwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo limeonekana kuwa na mvuto katika ulimwengu wa masumbwi baada ya Azam Tv kuingia makubaliano ya kuonyesha mubashara kutoka uwanja wa uhuru katika kipindi chote cha pambano hilo siku ya novemba 29 mwaka huu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya makubalinao kati Promota Jay Msangi na Mkurugenzi Mtendaji Azam Tv Tido Mhando, Promota Msangi, amesema kuwa asilimia kubwa maandalizi yamekamilika kuelekea pambano hilo.
Amesema kuwa pambano hilo litakuwa na msisimko kutokana na historia ya mabondia hao, kwani mfilipino Tinampay katika mapambano 50 aliyocheza hajawai kupoteza kwa nokauti.
Promota Msangi ameeleza kuwa ni bondia mzuri nchini Ufilipino, huku mtanzania Mwakinnyo akishika namba moja Afrika na Tanzania.
"Bondia Arney Tinampay anatarajia kufika nchini siku 13 kabla ya pambano, kabla ya pambano atakuwa anafanya mazoezi ya wazi katika maeneo tofauti ikiwemo Mlimani City, Mbagara pamoja na Tanga anapotoka bondika Mwakinyo" amesema Promota Msangi.
Amsema kuwa mashabiki 25,000 hadi 30,000 wanatarajia kuja uwanja wa uhuru kwa ajili kuona pambano hilo la kistoria, huku akibainisha kuwa hivi karibuni anatarajia kutoa taarifa kamili kuhusu utaratibu wa mashabiki kuingia katika mchezo huo.
Mkurugenzi Mtendaji Azam Tv Bw. Tido Mhando, amesema kuwa mchezo wa masumbwi Tanzania unapendwa na watu wengi hapa nchini.
Bw. Mhando amesema kuwa ni wakati mwafaka kumuona bondia Mwakinyo akitengeneza historia katika pambano hilo lenye mvuto ambalo litakuwa mubashara ili dunia kushuhudia.
"Lengo la Azam Tv kutoa burudani kwa wote kupitia mchezo mbalimbali ikiwemo masumbwi" amesema Bw. Mhando.
Kwa upande wake bondia Mwakinyo ametamba kuondoka na ushindi katika pambano hilo, huku akibainisha kuwa tayari ametumia masaa matatu kumsoma mpinzani wake.
Bondia Mwakinyo akimtandika Mwingereza Sam Eggington katika raundi ya pili.
Ameeleza kuwa jinsi nilivyojiandaa na pambano hilo.."sidhani kama Tinampay atafika raundi ya pili, kwa sababu mimi napenda sana kumpiga mtu kwa KO, hivyo natarajia kufanya hivyo hata kabla raundi ya pili haijaisha.”
Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni kuchapana na Tinampay anayeshika nafasi ya pili nchini kwao Ufilipino, kwenye pambano la raundi 10 la Super Water kilo 69.
Post a Comment