Ads

ZIARA YA DC MJEMA YAACHA MATUMAINI KIBAO KWA WANANCHI MBONDOLE,CHANIKA NA ZINGIZIWA.




Na John Luhende 
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema  ametoa wikimoja kwa  kwa  wataamu  wa  Manispaa na TAKUKURU   kufanya uhakiki wa matumizi ya shilingi milioni  100 ilyo tumika kujenga  zahanati ya Mbondole ili ujenzi huo uweze kukamilika wananchi waanze kupata huduma.

DC Mjema ametoa kauli hiyo alipotembelea kukagua ujenzi wa zahanati hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi  na ahadi  alizotoa katika ziara mwaka jana  pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo  amesema  jengo hilo halilingani na thamani ya fedha hiyo.

‘’ Nimekagua jengo hili  nimekuwa na shaka na fedha iliyotumika  na pia mradi umechelewesha ,agizo la Rais  ni kilamradi wa serikali kufanyika kwa wakati kwakuwa fedha ipo,pia nimeagiza mlinzi anayedai malipo yake ya miezi 20 alipwe na amenikabidhi funguo  za zahanati hiyo nimeona zilianchwa kinyume cha utaratibu “Alisema 

Aidha Mjema   amemwagiza afisa masoko wa Manispaa na uongozi wa soko la Gogo Chanika kugawa vizimba vya biashara kwa usawa na kusema kuwa wale wote waliotajwa kujihusisha na vitendo vya rushwa katika uagawaji vizimba  watachukuliwa hatua za kisheria  baadaya  uchunguzi kukamilika ambao ameagiza uanze maramoja.

‘’Kuna malalamiko mengi katika hilisoko  nasema kilamtu anahaki ya kufanya biashara popote hakuna cha uzawa kilamtu afanye biashara vyombo  vya nimeviagiza kufanya uchunguzi watu wote walitajwa kuwaumiza wananchi watachukuliwa hatua’’Alisema

Pia amewaataka wananchi wa kata ya Mbondole  walioamriwa na Mahakama kuondoka katika eneo walilovamia la Green  foundation  kulipafidia haraka ili wasije wakabomolewa nyumba zao kama inavyo eleza hukumu hiyo.

“Kutokana na hukumu ya Mahakama wananchi mlitakiwa mvunjiwe nyumba zenu lakini nilimuomba waziri wa Ardhi na mwekezaji tukaelewana mlipe fidia lakini nimesikia hapa kuna makundi matatu wengine wamekataa kulipa ,wengine wanalipa na wengine hawajamalizia madeni yao  mimi siwezi kuwalipia sinapesa hiyo naomba mlipe msije kuvunjiwa naomba wote wenye mogoro na green foundation tukutane ofisini kwangu “Alisema Mjema.

Pamoja nahayo DC Mjema  akisikiliza kero za maji elimu,maji  barabara na umeme  ametaka TANESCO  kuhakikisha  wananchi wa kata za  Chanika  na zingiziwa kuwa kabla ya mwezi December  watapata huduma hizo huku akiiagiza SUMATRA kuanzisha njia mpya ya daladala.

‘’Wanachi hawa wanataka huduma siyo maneno na ahadi za kila siku ,wafungiwe umeme haraka ,naomba wananchi kaeni na huyu mtu wa SUMATRA  mpange nataka mabasi ya kutoka karikoo chanika  na Posta yaanze wiki ijayo ,kama tuliweza pale kigogofresh sokoni ha huku hatuwezi kushindwa”Alisema 
 
Nao baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kutoa kero zao ,wameeleza kuhusu kero za maji ,ubovu wa barabara,ukosefu wa maji migogoro ya ardhi kuwa vimekuwa vikwazo kwa maendeleo na kumuomba DC Mjema kuzifanyia kazi.

No comments