WAZIRI KAIRUKI AIPA SIKU SABA TIC KUWAFIKIA WAWEKEZAJI WAZAWA
Meneja
wa Kiwanda cha kutengeneza Kahawa cha Wilaya ya Mbinga (MCCCO) Mhandisi Rabbian
Uromi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji)
Mhe.Angellah Kairuki kuhusu mitambo ya kutengeneza mifuko (magunia) ya
kuhifadhia kahawa katika kiwanda hicho kilichopo Mkoani Ruvuma wakati wa ziara
yake Septemba 23, 2019
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na
watumishi wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE kilichopo katika Wilaya
Mbinga alipotembelea kukagua mazingira ya wawekezaji nchini.Kulia aliyekaa ni
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe.Cosmas Nshenyi
...................................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala
ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) kutembelea na kugakua mazingira ya wafanyabiashara na
wawekezaji wazawa waliopo mkoa wa Ruvuma ndani ya siku saba.
Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua kiwanda cha
kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga cha MCCCO pamoja na kiwanda cha DAE kwa
lengo la kukagua mazingira na utendaji wa viwanda hivyo Mkoani Ruvuma.
Ziara hiyo iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Mhe.Christina Mdeme pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Viwanda, Wizara ya Kilimo, Wizara ya
Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, pamoja na baadhi ya taasisi za
serikali ikiwemo na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).
Waziri Kairuki alitoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa kituo
hicho hakijawafikia wawekezaji wazawa
kikamilifu hususani waliopo mikoani ili kuwatambua na kuwaelimisha kuhusu fursa
zinazotolewa na taasisi hiyo.
“Ninawaagiza TIC mfike
katika viwanda hivi ndani ya siku saba kuanzia sasa ili kuwatembelea na
kuwaeeleza huduma zinazotolewa na taasisi yenu ikiwemo fursa zilizopo na endapo
wataona inafaa wajisajiri kwa kuwa ni suala la
hiari,”alisisitiza Waziri Kairuki
Aidha alieleza kuwa ipo tija ya kuwatambua wawekezaji wazawa
waliopo nchini ka kuzingatia mchango wao katika uchumi wa viwanda kwa
kuzingatia mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji.
“Naelewa kuwa ipo miradi mingi iliyofikiwa na TIC zaidi ya
asilimia 72 hivyo niwatake mfike haraka mkoani Ruvuma hususan katika viwanda
hivi vya kahawa, ili kuvitambua na kueleza fursa na umuhimu wa kujisajili na
Taasisi hii ili kuendelea kuchangia na kuwa na tija zaidi katika uchumi wa
nchi,”alisisitiza
Mkurugenzi wa Sera Mipango na Utafiti wa TIC Mafutah Bunini
amesema katika kuboresha utendaji wao wamefungua ofisi za kanda saba ili
kuwafikia kwa urahisi wawekezaji wa ndani na kwamba wanaotoa uzito sawa kwa
wawekezaji wa ndani na nje.
“Na katika hili ndiyo maana viwango vya mitaji ya uwekezaji
vinatofautiana kwa wawekezaji wa nje na ndani ambapo mwekezaji wa ndani
anatakiwa awe na mtaji wa dola laki moja lakini mwekezaji wa nje ni dola laki
tano.
Naye Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya
Mbinga (MCCCO) amemuahakikishia Waziri kuwa wataendelea kuboresha mazingira
mazuri ya wafanyakazi na kuongeza thamani ya bidhaa zao za kahawa na
kuhakikisha jamii iliyowazunguka inanufaika na kiwanda hicho.
“tunaishukuru Wizara ya Uwekezaji kwa jitihada inazofanya za
kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyokuwepo
awali hali inayosababisha uwekezaji kukua kwa kasi”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha
kutengeneza kahawa cha DAE Bw. Danistan Komba ambaye pia ni mkulima wa kahawa
alimpongeza waziri kwa kutembelea kiwandani hapo na kueleza changamoto za
masoko ya kahawa na kuiomba Serikali kuendelea kuwaangalia wawekezaji hao
wazawa.
“Kipekee napongeza ujio wako, japo tunachangamoto ya masoko kwa
kuzingatia kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 36,000 kwa mwaka na kuuza
katika baadhi ya nchi,”alieleza Komba
Alifafanua kuwa, pamoja na changamoto za uhaba wa masoko,
kiwanda kimekuwa kikishiriki katika maonesho ya nchi zinazolima kahawa ikiwemo
Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi na Ethiopia.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye alieleza kuwa,
ziara hiyo imeleta chachu kwa wafanyabiashara na wawekezaji wazawa kwa
kuzingatia kuwa, Serikali imeahidi kutoa ushirikiano wa kina katika kutatua
changamoto zao ikiwemo kuwataka TIC kufika na kuwatembela katika muda
alioagiza.
Post a Comment