WAZIRI JAFO ATOA AGIZO ZITO KWA RC MAKONDA
NA HERI SHAABAN
WAZIRI wa Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Selemani Jaffo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar Salaam Paul Makonda kuitisha kikao cha zarula cha Bodi ya barabara Mkoa ili kutoa ufumbuzi kuhusiana na eneo la Mradi kisasa wa soko la Kisutu na Mradi wa Mwendokasi BRT ili visiathili miradi hiyo kwa muingiliano.
Waziri Jaffo alitoa agizo hilo wilayani Ilala leo wakati akikagua mradi wa soko la kisasa la kisutu kuangalia maendeleo yake na kuipongeza Halmashauri ya Ilala jinsi ujenzi unavyoendelea vizuri mradi wa serikali kuu.
"Nakuagiza Mchumi wa halmashauri ya Ilala Ando Mwakunga mumuandikie Katibu Tawala Mkoa kwa ajili ya kikao cha usuruhishi na Bodi ya Barabara mkoa,kiwakutanishe TANRODS ,BRT ,ofisi ya mkurugenzi na Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa soko kwa ajili ya kutatua changamoto iliyojitokeza katika muingiliano wa barabara ,daraja ,mradi wa BRT na soko alisema Jaffo.
Waziri Jaffo alisema kasi ya ujenzi inaendelea vizuri dhumuni la kikao hicho mradi wa mwendokasi kuweka kivuko cha watembea kwa miguu usiathili ujenzi wa soko la kisasa la wananchi hatua hiyo imefuatia wajenzi wa mradi kuwekewa vikwazo na TANRODS .
Aliagiza kikao hicho kifanyike ndani ya wiki mbili na kisha kupeleka taarifa hatua waliofikia.
Aidha alimwagiza Mkandarasi wa ujenzi huo mradi umalizike kwa wakati, kuarakisha ili zisingiliane na mvua za vuli.
Kwa upande mwingine Jaffo ameagiza apelekewe majina yote ya wafanyabiashara watakao fanyabishara katika soko hilo la kisasa .
Kwa upande wake Mchumi wa Halmashauri ya Ilala Ando Mwankunga alisema thamani ya mradi huo zaidi ya bilioni 13 fedha kutoka serikali kuu
Mpaka sasa Mkandarasi amelipwa bilioni 2.
Naye Msimamizi wa Mkuu wa Mradi huo,Ismail Mvungi alisema mradi huo unatarajia kumalizika mwaka 2020 Mwezi Agosti .
Mvungi alisema soko hilo lina vizimba 530 likikamilika thamani ya mradi wote shilingi bilioni 13.4
Post a Comment