FCS Yazindua wiki ya Asasi za Kiraia, Wajipanga kushirikiana na wadau.
Na Noel Rukanuga
Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS) imezindua wiki ya Asasi za Kiraia ikiwa na mipango mbalimbali ikiwemo kuongeza ubia, kujiimalisha, kushirikiana, pamoja kuongeza uwezo kwa asasi I5 ili kuhakikisha zinakuwa na mafanikio katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo tukio hilo limepewa jina la 'Wiki ya Azaki 2019' pamoja na kuzindua tovuti kwa ajili usajili kwa washiriki pamoja na kupokea mapendekezo ya tuzo ya asasi kwa ajili ya asasi bora kwa mwaka huu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Asasi za Kiraia Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Francis Kiwanga, amesema kuwa katika wiki ya asasi za kiraia wanatarajia kuongeza mafanikio katika utendaji wao katika kujadiliana masuala mbalimbali.
Bw. Kiwanga amesema kuwa asasi zitaongeza ushirikiano kwa wananchi, Bunge, Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
"Kwa mwaka huu tutaongeza wigo katika utendaji wa kazi pamoja na kuleta fursa za sauti za wananchi" amesema Bw. Kiwanga.
Bw. Kiwanga ameeleza kuwa mwaka huu wiki ya asasi ya kiraia imepangwa kufanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 4 hadi 8 Novemba 4-8 mwaka huu, huku akiwataka washiriki kujisajili katika tovuti.
Amesema kuwa taasisi I5 pamoja na serikali zitashiriki katika majadiliano ya kitu ya asasi ili kuleta tija katika utekelezaji.
Bw. Kiwanga amefafanua kauli mbiu ya wiki ya azaki 2019 ni 'Ubia kwa maendeleo: Ushirikiano kama nguzo ya maendeleo nchini Tanzania".
Katika uzinduo huo kulikuwa na wageni ambao ni Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta, Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt.Andrew Komba, Mwakilishi wa Taasisi zisizo za Kiserikali Bw. Timothy Mgonja, ambapo wote waipongeza FCS kwa kuratibu wiki ya Azaki.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta, Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt.Andrew Komba, amezipongeza Asasi za Kiraia kwa kazi nzuri wanayofanya.
Dkt. Komba amesema kuwa serikali inataka kuwe na umoja ili kujua utekelezaji wa majukumu ya kila Asasi za kiraia.
Dkt. Komba alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, ameeleza kuwa ili kufika malengo, asasi za kiraia zinatakiwa kuwa wazalendo na uwazi katika utekelezaji wa majuku yao.
"Serikali tumeandaa mfumo wa kusajili asasi za kiraia ili kujua yupo wapi na anatekeleza majukumu gani na kiasi gani cha fedha anacho" amesema Dkt. Komba.
Katika wiki ya Azaki patakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kupaza sauti na kuwezesha wa maneno ya ushirikiano na ufanyaji kazi baina ya watendaji wa serikali na wale wasio wa serikali.
Post a Comment