Ads

Waziri Hasunga aipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika



Mwambawahabari
NA HERI SHAABAN
WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga ameipongeza Tume ya Maendeleo ya  Ushirika Tanzania kutokana na uhamashishaji usimamizi udhibiti na ufatiliaji wa shughuli za ushirika na kuhakikisha vyama vya ushirika vinatekeleza majukumu.


Waziri Hasunga alisema Tume ya Maendeleo ya Ushirika iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuleta tija kwa wana Ushirika na jamii kwa ujumla.

Akizungumza katika  uwanja wa maonyesho ya Wakulima  Nyakabindi Simiyu katika siku maalum ya kuhamashisha ushirika  kupitia utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo awamu ya pili  (ASDB11) iliyotengwa kwa ajili ya kuandaa shughuli za ushirika mafanikio yaliopatikana na kuhamashisha wazalishaji kupitia sekta ya kilimo.

"Hadi kufikia mwezi mei 2019.nchi yetu ina jumla ya vyama vya ushirika 11,331vyenye idadi ya wanachama 4,611,804"alisema Hasunga.

Alisema wanachama watarajiwa 765 ,804 idadi hiyo imeongezeka kutokana na vyama vya ushirika 10,990 vyenye wanachama 2,619,311.

Aidha alisema kwa kipindi cha mwaka 2018 mpaka sasa jumla ya vyama vya Ushirika 341 vimeongezeka na wanachama 1,991,960

Pia alisema kufikia mwezi february 2019 Tume ilifanya ukaguzi mara kwa mara kwa vyama vya ushirika 3,140 sawa na asilimia 54 ya lengo la kukagua vyama 5,830.


Katika madhimisho hayo Waziri Hasunga alitoa vyeti  kwa kuvitambua vyama vya ushirika na taasisi zenye mchango katika sekta ya kilimo,uvuvi,na mifugo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandis Methew Mtigumwe amewashukuru Wakulima,Wafugaji na wavuvi kwa juhudi zao kubwa  za uzalishaji mazao  mbalimbali na alielezea umuhimu wa uzalishaji mazao mbalimbali kupewa  kipaumbele  na kuhusishwa katika masuala ya kilimo na Ushirika .

"Leo ni siku maalum ya kuhamashisha ushirika  kupitia utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo awamu ya pili  (ASDB11) iliyotengwa kwa ajili ya kuandaa shughuli za ushirika tunakupongeza Waziri Hasunga kwa uzinduzi wa Bima ya Mazao na kutoa vyeti vya utambuzi katika vyama vya ushirika na Wadau wa maendeleo ya sekta ya kilimo" alisema Methew.

MWISHO

No comments