Ads

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yawa kivutio Nanenane


Mkurugenzi wa kikundi cha Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akiwahudumia wateja katika maonyesho ya Wakulima Nanenane ndani ya banda la Ilala(Picha na Heri Shaaban)

NA HERI SHABAN,MOROGORO

BANDA la halmashauri ya Ilala limekuwa kivutio katika maonyesho ya 26  Kanda ya Mashariki  nanenane Mkoani Morogoro mwaka huu .


Akizungumza katika maonyesho ya 26 mkoni Morogoro leo Mkuu wa Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Esther Masome aliwataka wananchi kupita katika banda la halmashauri kujifunza kilimo cha kisasa ambacho akitumii udongo.

"Kilimo cha Lituce,hichi kilimo kipya mfumo  ndani ya mwezi mmoja na nusu zao linavunwa mboga mboga zinakuwa tayari "alisema Masome.

Masome amewataka wananchi kupita katika banda la halmashauli hiyo kujifunza kuhusiana na kilimo cha kisasa,kilimo cha magolofani  pamoja na utengenezaji wa Mkaa wa nishati Mbadala.


Aidha  Masome aliwataka wananchi kuja katika banda hilo kujifunza kilimo cha zao la mpunga  kwani kuna aina nyingi za zao la Mpunga ,mpunga wa asili na mpunga Chotara .

Alitaja sehemu ambazo zao la mpunga linastawi  vyema sehemu ya mabondeni zenye kutunza unyevu mwingi au katika kilimo cha umwagiliaji.

Pia alielezea zao la kilimo cha pilipili hoho halmashauri hiyo inalima  alitaja aina nne ya zao la pilipili hoho ,Yolo wonder,Calfonia wonder,emerald Giant .

Naye Mshiriki wa Maonyesho ya 26 katika banda la Ilala Mwenyekiti wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alimpongeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri kuwapa fursa Wanawake wa wilaya ya Ilala kutumia fursa hiyo kuja kufanya biashara .

Neema alisema yeye katika bidhaa zake za usindikaji anashughulika na bidhaa mbali ikiwemo Kalanga,Lishe,mboga  za majani na bidhaa mbalimbali.

Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kuwapa fursa  Wanawake wa wilaya ya Ilala   ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi

"Nawaomba Wanawake tuamke tutumie fursa hizi vizuri kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda" alisema Neema.


No comments