Ads

TBBF KUMSAKA MR. TANZANIA 2OI9




Na Noelukanuga, Dar es Salaam.
Mashindano ya kumtafuta Mr. Tanzania wa mwaka 2OI9 yanatarajia kufanya Novemba 29 mwaka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu wa Chama cha Watunisha Misuli Tanzania (TBBF) Bw. Francis Mapugilo, amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee kutokana maandalizi mazuri yanayofanyika.

Bw. Mapugilo  amesema kuwa katika mashindano ya mwaka huu wanatarajia kutambulisha ujio mpya ambapo watu watashindana ili kumpata Mr.Physique pamoja  Ms Fitness.

Bw.Mapugilo  amefafanua kuwa kutakuwa na ongezeko la madaraja hayo mawili ambapo ndani yake kutakuwa vipengere ambavyo ni Mr. Popular na Mr. Ms. Popular, Mr. Top mode, Mr. Extreme Fitness.

"Ms. Fitness ni daraja jipya ambalo Litawawezesha wasichana na wanawake kushiriki katika mashindano na kupata zawadi kwa Mazoezi magumu walioyafanya" amesema Bw. Mapugilo.

Ameeleza kuwa kwa upande wa washiriki katika nafasi ya  Mr. Physique ni wavulana walio na miili mipana yenye nguvu na mvuto unaotokana na ufanyaji wa mazoezi.

Mwenyekiti wa TBBF Bw. Nileh Bhatt, amesema katika mashindano hayo kila mshiriki atapata zawadi jambo ambalo litasaidia kuongeza hamasa.

Amesema kuwa mashindi wa kwanza atapata milioni tano huku mshindi katika katika kila kundi wakipata milioni 3, milioni 2, milioni I.

Mshauri katika Fitness Bi. Nasra Ishebabi, amesema kuwa ushiriki kwa wasichana katika mashindano hayo ni jambo la muhimu kwani kuna fursa nyingi.

Amesema kuwa wanataka kufanya mchezo huo kuwa chanzo cha kipato na ajira kwa vijana kwani mashindano hayo yanafanyika  dunia nzima

Amesema kuwa ni vizuri  kufanya mchezo huo kuwa chanzo cha kipato na ajira kwa vijana kwani mashindano hayo yanafanyika  dunia nzima .

"Nimekuwa nikiwashauri wasichana katika Mchezo huu katika kuhakikisha wanafanya vizuri"

No comments