Ads

RC MAKONDA AZINDUA MKAKATI "PEKENYUA TUKUFUKUNYUE" WA KUDHIBITI WAHAMIHAJI HARAMU MKOA WA DAR ES SALAAM*.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo August 29 amezindua *Mpango Mkakati wa kutokomeza Wahamihaji haramu* Mkoa wa Dar es salaam alioubatiza jina la  *"PEKENYUA TUKUFUKUNYUE"* na  kuwaagiza Watendaji wa Mitaa kurejesha *Daftari la Mkazi* ili Kila Mkazi kuanzia *ngazi ya Mtaa* afahamike *anapoishi na kazi anayofanya* jambo litakalosaidia pia kuondoa *uhalifu.*

*RC Makonda* amesema mpango huo ni *Mwarobaini tosha* wa kupambana na *Wageni wanaoishi Nchini kinyume na Sheria* na utahusisha Watendaji wa *Kata, Mitaa na Wananchi* ambao watakuwa na jukumu la *kutoa taarifa* pindi wanapobaini *uwepo wa mgeni au mtu wanaemtilia mashaka* kwenye Makazi wanayoishi.

Aidha *RC Makonda* amesema uwepo wa Wahamihaji Haramu Nchini ni jambo la *hatari kiusalama* kwakuwa baadhi yao wanafanya *uhalifu wa Wizi, Ubakaji, Uporaji, wanatumia rasilimali za nchi, wanatumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo Afya, Elimu na Ajira*, kusababisha *msogamano wa watu magerezani* pamoja na kuwa *Chanzo cha Migogo ikiwemo ya Ardhi*.

Kutokana na hilo *RC Makonda* ameviagiza *Vyombo Vyote vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Kata na Mitaa* kuhakikisha Mpango huo unafanikiwa kwa *100%.*

Kwa upande wake *Kamishina wa Uhamihaji Mkoa wa Dar es salaam* amesema wamebaini idadi kubwa ya wahamihaji haramu wanatoka mataifa ya *Burundi, DRC, Somalia na Ethiopia* na wamekuwa wakipendelea kuishi *Mkoa wa Dar es salaam kwakuwa umekuwa jiji lenye fursa nyingi za kibiashara.*

No comments