Ads

NDOA ZA UTOTONI BADO JANGA.

Na Mwandishi wetu
IMEKUWA jambo la kawaida ndani ya jamii ambapo baadhi ya familia wamekuwa wakiwaozeshama mabinti zao katika umri mdogo kwa sababu ya Mila na desturi kandamizi na zilizopitwa na wakati.

Hali hiyo ilikuwa ikisababisha wasichana wengi wenye umri mdogo kushindwa kuendelea na masomo, kutunza familia , kupata magonjwa hasa ya ngono huku wangine wakitelekeza familia kwa sababu ya kushindwa kuhimili changamoto za kifamilia.

Athari ya ndoa za Utotoni.
Athari ya ndoa za Utotoni ni zipi?
Ndoa za utotoni ni changamoto ya kiafya, kielimu, kijamii, na kimaendeleo. Kwa kuwa kiafya, kubeba ujauzito kabla ya umri wa miaka 20 huongeza hatari za vifo na ulemavu (kama vile fistula) kwa wasichana.

Ndoa za utotoni zinachangia kuongeza vifo vitokanavyo na uzazi na fistula kwa wasichana. Wasichana wanaoolewa katika umri mdogo wanakatishwa fursa za kujiendeleza kielimu na kuandaliwa kuwa nguvukazi bora kwa kukuza uchumi.

Pia, wasichana wadogo bado hawajawa tayari kisaikolojia kwa ajili ya majukumu ya kijamii ya kuwa wake na wazazi. Wasichana hawa hunyimwa fursa za kimaendeleo kama vile kujiendeleza kitaaluma na kushiriki katika ajira zenye vipato vya juu, kushika nafasi za uongozi, na kushiriki katika mabaraza ya kutoa maamuzi.

Ndoa za utotoni ni ukatili wa kijinsia na ni chanzo kimojawapo cha ukatili wa kijinsia, zinachangiwa na umaskini na ni mzizi wa umaskini.

Je, hali ikoje kwa Tanzania na nje ya nchi?

Kuna mikoa ya Tanzania ambayo kiwango cha ndoa za utotoni ni kikubwa, hasa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na baadhi ya nchi za Asia zina viwango vya juu vya Ndoa za Utotoni. Ambapo ripoti za Kitaifa na Kimataifa zinaashiria Hali ilivyo. I'm

Changamoto za Sheria.
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ni ya kibaguzi kwa kuwa inaruhusu wasichana kuolewa wakiwa katika umri mdogo (miaka 14 kwa idhini ya wazazi au walezi) na miaka 15 kwa ridhaa ya msichana mwenyewe.

 Sheria hiyo inaweka umri wa kuoa kwa mvulana kuwa ni miaka 18. Sharia hiyo inapingana na Sheria ya Mtoto, Sheria ya Elimu, na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (SOSPA).

Anasema kwa sababu hiyo, sheria zinazopingana na Sheria ya Ndoa zinawalinda wasichana walio mashuleni na kuwaacha walio nje ya shule.

Je, rika hiyo inastahimili mikikimiki ya ndoa?

Wasichana wadogo bado hawajawa tayari kimaumbile, kiafya, kimalezi, na kisaikolojia kwa ajili ya majukumu ya kubeba ujauzito na kujifungua, ya kuwa wake na wazazi, na yale ya kijamii.

Kuhusu upande wa uzazi, ushauri kwa Serikali na Wazazi?

Anaongeza kuwa erikali iangalie upya sheria zake ili kuinua umri wa ndoa kwa wasichana, kuondoa ubaguzi kati ya wavulana na wasichana, kuoanisha sheria zake, na kuwapa haki sawa wasichana wote walio shuleni na nje ya shule.

Anasema kuna umuhimu wa serikali kupanua wigo wa elimu au taarifa, ushauri, na huduma za afya ya uzazi kwa watoto ili wawe na uwezo wa kuamua kwa usahihi na kupata huduma stahiki zikiwezo za kinga na tiba.

Anasema pia, serikali iongeze juhudi za kuwawezesha wazazi kupata ujuzi wa malezi bora kwa watoto na kuwafanya washiriki kikamilifu katika kulinda haki na maslahi ya watoto. Wazazi nao wanapaswa kujali haki na usalama wa watoto wao wote, wa kike na wa kiume na kuepuka mambo yote yanayoweza kuhatarisha afya, uhai, na maendeleo ya watoto wao.

Anasema  Wazazi waiwajibishe serikali kuweka sera na sheria wezeshi na kugharimia kikamilifu utoaji wa huduma zinazotakiwa kwa ajili ya watoto wote.

Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana

Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana ni muhimu kama ilivyo katika maeneo mengine mengi ya maisha. Elimu au taarifa (information), ushauri (counseling), na huduma (services) kuhusu Afya ya Uzazi kwa Vijana ni muhimu kutokana na mahitaji ambayo Vijana wanayo na pia ni haki zao za msingi kama zilivyoainishwa katika Katiba, Dira ya Maendeleo, Sera, Mipango, na Mikakati ya nchi yetu.

"Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana inahusu kuwapa maarifa ya kujitambua, kujua mfumo wa uzazi na mabadiliko yanayotokea katika maisha yao wanapoendelea kukua, namna ya kufanya maamuzi sahihi, changamoto wanazoweza kukabiliana nazo, na namna ya kuzikabili,"anasema Mlali.

Anaongeza kuwa, Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana ni maarifa kuhusu maisha, afya, na maamuzi muhimu.

Anasema vijjana wakipata taarifa sahihi kuhusu Afya ya Uzazi, Ushauri kwa wakati mwafaka, na huduma stahiki wataweza kukua vema na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kutimiza malengo yao katika maisha.

Changamoto ambazo vijana wanakutana nazo ni nyingi. ya kwanza ni kukosekana kwa mada za elimu hiyo kwenye mitaala  rasmi ya elimu.

Anasema inamaanisha kwamba vijana wanaachwa kujielimisha wenyewe bila miongozo sahihi na ya wazi. Matokeo ni kwamba wanaangukia kwenye taarifa zisizo sahihi na kupata madhara kama vile kuanza ngono mapema na katika mazingira yasiyokubalika.

"Hiki ndicho chanzo cha mimba za utotoni, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI, utoaji wa mimba, uzazi katika umri mdogo, fistula, kufukuzwa shule, msongo wa mawazo, na hata mauti,"anasema Mlali.

Ushauri na huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana pia zinapatikana kwa kiwango kidogo sana na kwa viwango duni. Hizi ndizo zongwsaidia kwa kinga na tiba kwa Vijana. Hadi mwaka 2015 ni vituo vitatu tu kati ya kila vituo kumi vya huduma za afya vilikuwa na uwezo wa kutoa huduma rafiki kwa Vijana.

Anasema Serikali inakusudia kuongeza idadi hiyo hadi kufikia vituo nane kati ya kila vituo kumi ifikapo 2020. Hata hivyo, utashi wa watoa maamuzi bado ni mdogo na bajeti kwa ajili ya huduma hizo bado ni finyu kufikia lengo hilo.

Kuna haja ya kurekebisha mitaala, kuongeza bajeti, na kuongeza idadi ya watoa huduma wenye ujuzi wa kutoa huduma rafiki kwa vijana ili kukabiliana na changamoto hizo.

Pia kutimiza malengo ya taifa ya kuwaandaa Vijana kuwa na afya bora na kuwawezesha kutimiza malengo yao katika maisha.

Kwa upande wake, Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Makao Makuu ya Polisi, Mohamed Mcheu anasema, ndoa za utotoni ni changamoto inayochangiwa na malezi ya upande mmoja, umaskini na ukosefu was taarifa sahihi kuhusu afya ya uzazj.

"Malezi yanachangia ndoa za utotoni kuzidi kuknhezeka siku dadi siku,"anasema Mcheu.

Mcheu anasema, sheria zilizopo ya Ndoa na ile ya Elimu zinahitajima maboresho kwakuwa nyingine inataja umri sahihi was kuolewa kwa makubaliano ya Wazazi huku nyjngine ikitaka Hadi afikishe miaka 18 ndio anaweza kuolewa.

Meneja Kitengo Cha Uchunguzi was Saratani na Elimu kwa Umma (ORCI),kutoka Taasisi ya Saratani, Dk.Maguha Stephano anasema, athari za kufanya mapenzi katika umri mdogo ni nyingi  ikiwamo kupata Saratani ya mlango wa kizazi.

Anasema tafiti nyingi zinaonyesha takwimu za Saratani ya mlango wa kizazi inawapata wasichana wenye umri wa miaka 30 hadi 50 ndio waathirika wakubwa.

Maguha anasema takwimu zinaonyesha Kati ya watu 100 wanaopima Saratani 33 hubainika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

"I'll kudhibiti saratani hi ya mlango wa kizazi tumeamua kutoa chanjo kwa mabinti wenye umri wa miaka 9 hadi 14.

Anasema.wasichana wanaolewa mapema wapo hatarini kupata .maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.

"Msichana anayeolewa mapema au kuanza mapema kufanya mapenzi yupo mbioni kupata maambukizi ya saratani,"anasema Maguha.

No comments