Meya Kumbilamoto atoa neno zito kwa walemavu.
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, ameitaka jamii kuwaungamkono watu wenye ulemavu katika kazi zao ilikuwasaidia kujikimu kimaisha na kuacha utegemezi kwa kuomba omba mitaani.
Meya Kumbilamoto ametoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa album ya nyimbo za injili inayo julikana kwa jina la Kalipia gharama zote , ya mwimbaji Steven Mkami ambaye ni kipofu, huku akimtaka mwimbaji huyo kutokata tamaa ya maisha serikali imeweka utaratibu wa kuwasaidia walemavu.
“Naomba wadau wa maendeleo waweze kumsaidia huyu kijana ameamua kutumia kipaji chake kumwimbia Mungu angeweza hata kuimba nyimbo za kidunia ( Bongoflava ) lakini ameona kunamaisha baada yamaisha haya nay eye anatafuta Paradiso“Alisema
Kumbilamoto kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Ilala mhe.Sophia Mjema wameweza kumsaidia mwimbaji huyu jumla ya shilingi 500,000 ambapo ametumia fursa hiyo kuwahimiza walemavu kujiunga katika vikundi ili waweze kufaidika na mikopo inayotolewa na Manispaa badala ya kubaki wakiomba omba mitaani.
“Tunamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuweka mikopo ya asilimia mbili kwa walemavu sasa wanaweza kukopeshwa na kufanya kazi zao kwa uhuru na omba nitoe wito kwa walemavu wote ,waige mfano wa Steven Mkami angeweza kuchukua kopo na kwenda mnazi mmoja kuomba lakini akaamua kutumia kipaji chake “Alisema Kumbilamoto.
Kwa upande wake Steve Mkami amewaomba watu wote wenye mapenzi mema kumsaidia ili awe na makazi aweze kufanya kazi zake uimbaji kwa uhakika kuliko hivi sasa ambapo amesema anapanga.
“Mimi nilianza uimbaji mwaka 2012 nilianza uimbaji ,kwa wale ambao hawanifahamu mimi nilizaliwa nilikuwa naona lakini nilizidishiwa dawa ya kwinini macho yakapata presha hatimaye nikashindwa kuona ,ninachohitaji kwasasa ni msaada kuhusu makazi nina familia na watoto nina yeyote atakaye guswa anaweza kunisaidia’’Alisema Mkami.
Aidha Mkami amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kuwa na ushirikiano na kusema kuwa waimbaji hao wamekuwa hawana ushirikiano ukilinganisha na waimbaji wa nyimbo za kidunia ,huku akidai kuwa hata yeye alialika baadhi ya waimbaji lakini wamekuwa wakitaka kupewa fedha ilikushiriki naye katika uzinduzi.
Nao baadhi ya waalikwa waliofika kuchangia uzinduzi huo wamepongeza hatua ya mwimbaji huyo na kumshukuru Mungu kwa kuwa amempa ujasili wam kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia kipaji chake .
“Tujifunze kwa Yesu mwemyewe alikuja kutusaidia sisi tukiwa wenye dhambi kwahiyo tusijali kwamba labda huyuniadui yangu bali tuwatendee mambo mema ‘Alisema Donald Mushi.
Post a Comment