KOCHA MATOLA AJIPANGA KUIPA POLISI TANZANIA UBIGWA LIGI KUU.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao kilimo cha Busega Mazao LTD kilichppo mkoani Simiyu Deogratius Kumalija(katikati) waki
Na Francis Peter, Dar es Salaam.
Kocha mpya wa timu hiyo Selemani Matola amesema mbinu alizozitumia katika timu yake ya dhamani ya Lipuli atazidisha zaidi katika kutoa ujuzi katika huduma yake katika kikosi hicho kuhakikisha kina kuwa tishio katika Ligi Kuu msimu huu.
Kikosi cha Polisi Tanzania kilichopanda daraja msimu huu kinamuonekano wa matarajiwa mema,tayari ratiba inaonesha Ligi Kuu Tanzania Bara itaanza rasmi Agosti 23, mwaka huu huku maafande hao wakitarajiwa kufungua dimba dhidi ya Coastal Unioni ya Tanga kwenye uwanja wa Ushirika Moshi,Kilimanjaro.
"Wachezaji wanafikia asilimia 99 , waliosajiliwa katika kikosi changu ni wale niliowapendekeza lakini bado naendelea kuwatizama kupitia mechi za kirafiki nataraji watakuwa fiti kabla ya kuanza ligi,"anasema Matola.
Matola anasema wachezaji halionao ni wazuri kutengeneza kikosi cha ushindani licha ya upya wa timu ila timu pinzani zitarajie kupata shida kwani anahakikisha anakijenga kikosi katika ari nzuri ya ushindani.
Mdhamini aliyeipandisha dararaja mkurugenzi wa kampuni ya kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao kilimo cha Busega Mazao LTD kilichppo mkoani Simiyu Deogratius Kumalija, amesema kuwa kikosi hicho kimepanda daraja hakitakuwa kichwa cha mwendawazimu ,kama uongozi wa juu wa serikali unavyosisitiza kuwa wangependa kuona udhamini unaleta tija katika kusaidia kupata matokeo mazuri.
Kumalija ametoa wito kwa wananchi kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini,pia amewataka wakazi wa Wilaya hiyo ya Busega na Mkoa kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanazalisha kwa wingi mazao yote yanayotakiwa katika kiwanda hicho ukiwepo mpunga na mahindi kwa kuwa kitatoa soko la uhakika na kupelekea ongezeko la pato la mtu mmoja mmoja.
Post a Comment