Ads

Manispaa ya Kinondoni yaanza ujenzi wa mradi wa coco Beach

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kuanza ujenzi wa utekelezaji wa mradi wa fukwe ya Osterbay maarufu 'Coco beach' mwezi wa 9 mwaka huu ambao gharama yake ni shillingi bilioni I4.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar es Salaam. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta, amesema kuwa mradi wa Coco beach unatarajia kukamilika ndani ya miezi sita baada ya mkandarasi kuanza kazi.

 Mhe. Sitta amesema kuwa utekelezaji wa wa mradi wa Coco Beach ulianza kwa kumtafuta mtaalam mshauri kwa ajili ya kupitia michoro iliyokuwepo awali, kuandaa taarifa za athari za kimazingira, uandaaji wa nyaraka za zabuni pamoja na kufanya usimamizi wa ujenzi.

"Mei 2 mwaka huu Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitangaza zabuni ya kuwapata waonesha nia kwa ajili usimamizi wa ujenzi wa fukwe ya Coco" amesema Mhe. Sitta.

Mhe. Sitta amefafanua kwa kuzingatia uharaka wa ujenzi wa mradi huo, mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa uendelezaji wa fukwe ulianza kwa kupitia mchora wa mradi kwa mara ya pili.

"Kwa sasa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ina michoro sahihi yenye gharama ambayo ipo ndani ya bajeti iliyoombwa toka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu" amesema Mhe. Sitta.

Amesema kuwa tayari nyaraka za zabuni zimekwisha tolewa kwa wakandarasi waliodhinishwa ambao wanatarajiwa kurudisha nyaraka hizo mwezi August I9 mwaka huu.

Hata hivyo August 9 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  alitoa Mwezi Mmoja kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa maboresho ya *Fukwe za Coco* unaanza *mara moja* na kama wakishindwa *watanyang'anywa fedha hizo* na kutafutwa mzabuni.

No comments