KUMBILA MOTO AFUFUA MATUMAINI YA NDOTO ZA KIJANA MLEMAVU ALIYETESEKA KWA MIAKA MINGI.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Kijana
mmoja anayejulikana kwa jina la Deugratius Francis Sangawe amewaomba
wasamilia wema kumsaidia ,ili awezekupata namna ya kujipatia kipato baada
ya kupata ajali ya pikipiki na kupata ulemavu wa kudumu.
Deuogratius alitoa
ombi hilo katika mkutano wa kupongeza diwani wa kata ya vingunguti Omary
Kumbilamoto pamoja na kutoa mafunzo kwa wajasiliamali ulioandaliwa na wanachi
wa kata hiyo ,ambapo amemshukuru Kumbilamoto kwa msaada aliompa.
“Namshukuru
sana Meya kwa moyo wake wa kujali mimi
nilipata ajali miaka mingi nimekuwa ndani bila msaada sijiwezi kutembea leo
amenipatia baiskeli (Wheel chair) itaniwezesha sasa kutekeleza majukumu yangu
katika kufanya kazi maana mikono ninayo tatizo nimiguu”alisema
Katika
mkutano huo Kumbilamoto ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ilala ,amesema
mkutano huo uliandaliwa bila ya yeye kuelezwa nini atafanyiwa na
amewashukuru wananchi hao kwa moyo huo lakini naye aliandaa msaada baiskeli kwa mlemavu yenye thamani ya shilingi
400,000 pamoja na jiko la Ges .
“Nawashukuru
sana wananchi wa Vingunguti sikujua kuwa jambo hili litakuwa kubwa namna
hii,nashukuru kwa kunijali na kutambua mchango wangu ningali hai ,wengi
tumezoea mtu anapo kufa ndiyo anakumbukwa “alisema
Hata
hivyo Kumbilamoto amewataka viongozi
nchini kuiga mfano wa uchapakazi wa Rais Magufuli ili
kuleta maendeleo kwa taifa .
“Haya
tunayafanya kumuunga mkono Rais wetu yeye hapumziki kuwatumikian watanzania
hatabakiwa ameenda Chato kupumzika utasikia tu anafanya jambo fulani amekuwa mfano wa kuigwa ,tangu ameingia
madarakani ametekeleza ahadi zake nyingi alizo waahidi watanzania “alisema .
Naye mwakilishi
wa Boda boda kata ya vinguti alikuwa amemtaka kijana huyo kuichukulia hali yake
kama fursa,na kusema kuwa kata hiyo
imepata kiongozi mchapa kaqzi na anaye yali wananchi wake kwani amekuwa msaada
kwa wananchi kwa kilajambo anapo hitajika .
“Sisi
tumejaribu kwa kilahali kumsaidia mwananchama wetu baada ya kupata ajali lakini
kipato chetu ni kidogo tunakila sababu
ya kumshukuru Diwani kwa msaada mkubwa huu alio utoa na si tunaaahidi tutaendelea kusaidiana naye
kwa kila hali”alisema mwenyekiti huyo.
Pamoja na hayo
,afisa Vijana Manispaa ya Ilala Sapicia
Masaga ameahidi kumtafutia kikundi
kijana huyo ili aweze kuunganishwa katika mikopo ya bajaji wanazo patiwa
walemavu aweze kuendelea na kazi zakiuchumi.
“Usihuzunike
sana kupata ulemavu siyo mwisho wa maisha Manispaa
imekuona tua kuahidi kuwa hatutakuacha tutakuwa nawe begakwa bega nimekuona
bado munao uwezo mkubwa wa kufanyakazi tena ulikuwa dereva tutakukopesha
bajaji itakusaidia maana mikpo hii ya
serikali haina riba natumani utaweza “alisema Masaga.

Post a Comment