Jumuiya Ya Wazazi Kata Ya Mburahati kujenga ofisi Ya Kata CCM, Yatoa msaada kusaidia elimu.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mburahati jijini Dar es Salaam wametakiwa kuendelea kuwa na umoja katika utekelezaji wa majukumu jambo ambalo litasaidia kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua shina la CCM Mburahati pamoja na kufungua harambee ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mburahati, Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Bw. Chifu Sylvester Yared, amesema kuwa umoja wa wazazi Kata ya Mburahati ni mfano mzuri katika utekelezaji.
Bw. Yeledi amesema kuwa umoja ni nguzo muhimu katika kufika malengo kwa kushirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza irani ya CCM kikamilifu.
"Umoja wa Wazazi Kata ya Mburahati mmefanya kazi nzuri, naomba ofisi hii ya kata ikatoe huduma kwa watu wote" amesema Bw. Yeledi.
Bw. Yeledi alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shina la CCM Mburahati ambapo alichagia shilingi laki moja ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata Ya Mburahati Bw. John Mapunda, amesema kuwa ujenzi wa Ofisi ya Kata umekuja kutokana na changamoto ya ukosefu ya eneo la kufanyikia kazi kwa CCM katika kata hiyo.
Bw. Mapunda amesema kuwa wajumbe
walikuwa wanapa shida eneo la kufanyika kazi za chama hasa ukizingatia kuna uchaguzi wa Serikali za mtaa unakaribia.
"Ili kufanikisha ujenzi wa ofisi ya CCM Kata Ya Mburahati leo tumeamua kufanya harambee ili kupate fedha za kukamilisha ujenzi" amesema Bw. Mapunda.
Bw. Mapunda amesema kuwa ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Mburahati unatarajia kukamilika kabla ya tarehe I, 9 mwaka huu.
Kaimu Katibu wa CCM Kata ya Mburahati Bw. Mike Sangu, amesema kuwa katika kipindi cha uongozi CCM wamefanikiwa kukamilisha miradi mbalimbali katika kata ya Mburahati.
Bw. Sungu amesema kuwa miongoni mwa vitu vilivyotekelezwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, zahanati pamoja na huduma za maji katika kata ya Mburahati.
Katika hatua nyengine Jumuia ya Wazazi Kata ya Mburahati imefanya ziara katika maeneo tofauti ndani ya kata hiyo ikiwemo tawi la CCM Mburahati Kisiwani pamoja na kituo cha polisi.
Wakiwa katika tawi la Mburahati Kisiwani wamefanikiwa kuchangia mifuko ya saruji na rangi kwa ajili kukarabati Shule awali ambayo ipo eneo hilo.
Hatua ya kuchangia mifuko ya saruji na rangi katika Shule hiyo imekuja baada ya kuona watoto wakisoma katika mazingira ambayo sio rafiki.
Imeelezwa kuwa Jumuia ya Wazazi kata ya Mburahati wanapenda kuona wote wakisoma katika mazingira rafiki na kupata elimu bora pamoja na kuwa na nidhama.
Kutokana na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano, leo zaidi ya watu watano wamejiunga na CCM wakitoka vyama vya upizani, huku wakibainisha sababu ya kuhamia CCM ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Post a Comment