Harmonize aiandikia WCB kujiondoa.

Meneja wa kundi la Wasafi, Sallam amesema msanii Harmonize kwa sasa ndani ya moyo wake hayuko WCB, isipokuwa tu yupo kimakaratasi na tayari ameshaandika barua ya komba kuvunja mkataba na kundi hilo.
Akizungumza
na Wasafi TV, Sallam amesema hata katika tamasha la Wasafi
lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafs na
kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa ameshajitenga na WCB.
“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.
“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.
“Sisi
katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu
kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia
usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam na kuongeza;
“Harmonize ameshatuma barua ya maombi Wasafi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote.
Post a Comment