Ads

MTANZANIA MONALISA AZUNGUMZIA SAKATA LA WANAHARAKATI TZ.


Mtanzania Bi Monalisa Ndala akizungumza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mtanzania Bi Monalisa Ndala ametoa wito kwa uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwachukulia hatua wanaharakati wanaotoa lugha ambazo sio rafiki ambazo zinalenga kuwachafua viongozi mbalimbali wakiwemo  watumishi wa mungu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Bi Ndala amesema kuwa kuna wanaharakati wamekuwa wakivunja Sheria za nchi bila kuchukuliwa hatua kitu ambacho sio kizuri katika nchi.

Amesema kuwa viongozi wastaafu wamekuwa wakitolewa lugha sio nzuri  jambo ambalo linaweza kuleta mpasuko kwa kuwa na makundi ambayo hayana tija kwa taifa.

Bi Ndala amefafanua kuwa kama mtanzania anaona sio jambo jema mambo yanayozungumzwa na wanaharakati hao yakaachwa bila kuchukuliwa hatua.

"Wito wangu kwa marais wastaafu, viongozi kuzungumzia tuhuma zinazozungumziwa juu yao ili kuondoa zitofahamu." amesema Bi Ndala.


No comments