MCHUNGAJI MASHIMO ATOA NENO LA UNABII USHINDI WA SIMBA DHIDI YA AS VITA
Mchungaji wa Mitume, Manabii na Maskofu Tanzania Mchungaji Komando Mashimo ameitaka klabu ya Simba kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za dini zote katika kuhakikisha zinafanya maombi ili timu hiyo iendelee kufanya vizuri katika michuano ya klabu Bigwa Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mchungaji Mashimo, amesema kuwa watanzania wanapenda kuiona klabu ya Simba inafanya vizuri jambo ambalo lilipelekea baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kumuomba afanye maombi ili washinde katika mchezo wao dhidi ya As Vita kutoka kongo.
"Viongozi wa Simba wanatakiwa watushirikishi viongozi wa dini zote katika kufanya maombi ya kuiombe timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri katika michuona ya klabu bigwa afrika tofauti na hapo itakuwa ni vigumu kuchukua kombe hilo" amesema Mchungaji Mashimo.
Katika hatua nyengine ameeleza kuwa anamshukuru mungu kwa kuendelea kutoa unabii, kwani kabla ya mchezo wa Simba aliweza kubainisha kuwa Simba atashinda magoli mawili.
Machi I6 mwaka huu timu ya Simba iliandika historia ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Walikuwa ni Vita walioanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Kazadi Kazengu mnamo dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza na baadaye Simba wakasawazisha kupitia kwa Mohammed Hussein mnano dakika ya 36.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake na Simba wakipigana kusaka bao la pili ili kupata nafasi ya kuingia hatua ya Robo Fainali.
Jitihada za Simba kusaka bao zilifanikiwa baada ya kosakosa nyingi langoni kwa Vita ambapo Clatous Chama alifanikiwa kupachika bao la pili kwenye dakika ya 90 ya mchezo.
Bao la Chama limeweza kuipa Simba historia mpya ya kutinga hatua hiyo kwa bao la Chama ambaye pia aliiwezesha kutinga hatua ya Makundi alipofunga dhidi ya Nkana walipocheza Uwanja wa Taifa na matokeo yakiwa ni 3-1.
Msimamo wa kundi D uliaonesha Al Ahly walioungana na Simba kufuzu nafasi ya kwanza wakiwa na alama 10 baada ya kuitandika JS Saoura mabao 3-0.
Simba nao baada ya ushindi walifanikiwa kumaliza wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama 9 huku Saoura wakiwa nafasi ya tatu na alama 8 pamoja na AS vita wakiwa wa nne na alama 7.
Post a Comment