WAZIRI MKUU AFUNGA SOKO LA NDUTA
Mwambawahabari
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amefunga soko la wakimbizi na wananchi
lililoanzishwa nje ya kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani
Kigoma.
Hatua
hiyo imekuja baada ya soko hilo kubainika kuwa chanzo cha wakimbizi
kutoka nje ya kambi kiholela na kushiriki katika kufanya matukio ya
kiharifu.
Waziri
Mkuu ametangaza uamuzi huo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati
akizungumza na watumishi wa umma katika ya Halmashauri ya Kibondo.
”Vitendo
vya uhalifu wilayani Kibondo vikiwemo vya utekaji wa watoto
vimeongezeka na kusababisha hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.”
Waziri
Mkuu amesema ni vema halmashauri hiyo ikaandaa utaratibu wa kutoa
vibali vitakavyowaruhusu Watanzania kupeleka bidhaa ndani ya kambi
hivyo.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewataka wananchi waliopewa dhamana ya kufanya kazi kwenye
kambi za wakimbizi wawe waadilifu na wasimamie sheria.
“Nafahamu
tunao watendaji wetu ambao wapo kambini kusimamia shughuli mbalimbali
za wakimbizi, tekelezeni wajibu wenu ipasavyo na si vinginevyo.”
Baada
ya kuzungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Kibondo, Waziri
Mkuu alikwenda wilayani Kakonko na kukagua mradi wa maji Muhange.
Pia
Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa makao makuu ya
Halmashauri ya wilaya ya Kakonko unaotarajiwa kugharimu sh. bilioni
4.5.
Post a Comment