MALKIA WA TEMBO ATUPWA JERA MIAKA I5
Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu raia wa China, Yang Feng Glan (75) maarufu kama Malkia wa tembo, na wenzake Wawili kutumikia kifungo Cha miaka 15 gerezani kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 13, kinyume cha sheria.
Pia katika shtaka la pili, washtakiwa wote hao wamehukumiwa kwenda jela miaka miwili au wakishindwa watatakiwa kulipa faini ya zaidi ya Bilioni 27.
Mbali na Feng washtakiwa wengine waliohukumiwa ni wafanyabiashara raia wa Tanzania, Salvius Matembo na Philemon Manase, ambao wote walikuwa wakitetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Hassan Kiangio.
Mbali na Feng washtakiwa wengine waliohukumiwa ni wafanyabiashara raia wa Tanzania, Salvius Matembo na Philemon Manase, ambao wote walikuwa wakitetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Hassan Kiangio.
Post a Comment