Waziri Lugola afika katika kaburi la Kijana aliepigwa risasi Kituo cha Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amefika nyumbani kwa kijana Richard Peter, ambaye amefariki siku za hivi karibuni kwa kupigwa risasi akiwa katika kituo cha polisi.
Akizungumza
mbele ya familia hiyo ambapo alifika kwa ajili ya kutoa salamu za pole
kutoka kwa Rais wa Magufuli, Lugola amesema polisi linaendelea na
uchunguzi juu ya tukio hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.
Lugola
amesema; “ Rais alipopata taarifa zilimshtua na sababu moja kubwa ya
kumshtua ni kwamba amefia kwenye eneo la polisi, kwa hiyo amenituma
niwapeni pole sana”
"Niwaombe
watanzania mliamini jeshi la polisi maana si jehi la kuua watu na wala
hatufundishi askari wetu kuua watu kwa hiyo isitafsiriwe jeshi letu ni
la kuua watu muwe nasubira" .Ameongeza Kangi Lugola.
Waziri
huyo kwa sasa yuko ziarani Mkoa wa Arusha ambapo siku ya kwanza
alizungumzia kuhusiana na tukio la kushambuliwa na Tundu Lissu pamoja na
kuzungumza na madereva wa bodaboda mapema jana.
Post a Comment