KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU.
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Wajane na waleva waishio kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala , wametakiwa kuwa na umoja
na ushirikiano ilikuweza kufanya
biashara ndogondogo zitakazo wasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku na
kumudo kurejesha fedha za mikopo ambayo
wanatarajiwa kukopeshwa na Manispaa.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbila moto wakati wa mafunzo mafupi ya ujasilia mali yaliyofanyika chini ya Maafisa mikopo na Afisa vijana wa
Manispaa ya Ilala , ambapo pia
amegawa Mikate 400, kwa makundi hayo.
Aidha kumbilamoto
ameitaka jamii kuto yanyanyapaa makundi hayo kwakuwa kufanya hivyo ni kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu.
“Makundi ya yatima wajane na walemavu alisisitiza sana
Mwenyezi Mungu tuyatazama sana kwa jicho
la huruma na kuya saidia hivyo nawaomba
sana viongozi wenzangu kwa hali na mali
tujitolee misaada , nashukuru pia kama
manispaa tumetenga takribani million 700
kwaajili ya mikopo “Alisema Kumbilamoto.
Mwamba wa habari pia imezungumza na Makundi yote yaliyo hudhuria
mafunzo hayo ambapo Ester Toi Nzigo, ambaye anatoka kundi la Mama wajane amesema mikopo hiyo itawasaidi kwakuwa ninafuu
kuliko hapa awali ambao mikopo hiyo ilikuwa inatolewa kwa Riba kubwa .
“Tuta mudu kulipa mikopo hii kwa kuwa tumesha zoea kulipa
mikopo riba tutapata unafuu mkubwa tuna
mshukuru sana Diwani wetu Kumbilamoto ,Rais Magufuli na Makamu wa Rais Mama
Samia, alituahidi kuwa wananawake tutapewa mikopo sasa yametimia “Alisema
“Sisi walemavu mikopo hii itawasaidia kuondokana na hali ya
kuomba omba mitaani sasa tutakuwa na biashara zetu “Alisema Fides
Mwakilema .
Post a Comment