WAZIRI KAIRUKI: SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI NA ENDELEVU KATIKA SEKTA YA KILIMO.
Mwamba wa habari
NA.
MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria
kuendelea kujenga mazingira wezeshi na endelevu katika Sekta ya Kilimo kupitia sera imara na zenye kutekelezeka.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki wakati akifungua Kongamano la Tano la Wadau wa Sekta ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Sera Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 13Februari, 2019.
Waziri alieleza
kuwa, dhamira ya Serikali inaenda sambamba na mchango wa sekta ya Kilimo katika
uzalishaji pamoja na ukuaji wa uchumi nchini kwa kuzingatia namna sekta hiyo
inavyochangia katika maeneo mengi ikiwemo,utoaji wa ajira kwa wananchi
waliowengi.
“Ni
mambo ambayo yanajieleza yenyewe na kila mmoja wetu anayajua vizuri. Asilimia 65.5 ya Watanzania wanategemea ajira
na maisha yao kwenye kilimo, pia kinachangia asilimia 95 ya mahitaji ya chakula
nchini na asilimia 65 ya mali ghafi ya viwanda vyetu,”alisema Kairuki
Aidha
aliongezea kuwa, asilimia 30 ya fedha za kigeni hutokana na mauzo ya nje ya
mazao na bidhaa za kilimo na huchangia asilimia 25 kwenye
pato la Taifa.
Sambamba
na hilo waziri alieleza kuwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano tangu
imeingia madarakani imeendelea kutambua umuhimu wa kilimo katika kuongeza tija
maeneo ya uzalishaji na mna haja ya kuleta msukumo zaidi katika kukiendeleza.
Pamoja
na jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta hiyo, Waziri alibainisha baadhi
ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo na sehemu kubwa ya kilimo
kutegemea jembe la mkono, matumizi madogo ya mbegu bora zinazotoa mazao mengi
na kuhimili maradhi na athari za kimazingira, matumizi ya maji ni kidogo mno
pamoja na kilimo kutegemea mvua bila
kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji chenye uhakika.
“Tunategemea
mno mvua ya Mwenyezi Mungu hatujatumia vya kutosha maji aliyotuwekea juu ya
ardhi na chini ya ardhi kwa kilimo katika hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo
nchini hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha kumwagilia lakini ni asilimia 1
tu ya ardhi hiyo inamwagiliwa. Tumejipa lengo la kuongeza kilimo
kinachomwagiliwa nchini,”alisisitiza Kairuki
Kairuki
alihamasha wakulima kuendelea kutumia mbolea kutokana na Tanzania kutumia
wastani wa kilo19 kwa hekta kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha kiwango cha
takribani kilo 50 kwa hekta kinachotumiwa na Jumuiya na Nchi za Kusini mwa
Jangwa la Sahara.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Kilimo, Mhe.Omari Mgumba alieleza jitihada za serikali
kuendelea kuhakiki madai ya madeni yenye ukakasi ya Wakala wa pembejeo
wanaosambaza mbegu na mbolea wanaoidai serikali kiasi cha shilingi bilioni 35.
“kama
mnavyofahamu mwaka ukipita wa fedha madeni yanahamia Wizara ya Fedha kwa hatua
zingine ikiwemo kuyachunguza na kujiridhisha ambapo hadi sasa yamebainika kuwa
na ukakasi katika takwimu na tofauti ya taarifa na Serikali inaendelea
kufuatilia hujuma zilizofanyika ili kujiridhisha,”alisisitiza Mgumba.
Naye
Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Chuo cha Kilimo cha Sokoine ,Jackline Mkindi
alipongeza uwepo wa kongamano hilo ambalo litatoa fursa za kujadili na kueleza
changamoto wanazokumbana nazo hususani upande wa usambazaji wa Pembejeo nchini na madeni yaliyopo ambayo hadi sasa ni
sh.bilioni 39.9 ambazo zinapaswa kulipwa na serikali.
“Tunaimba
Serikali ishushe bei na kuendelea kulipa madai sahihi kwa wanao stahili pamoja
na kutataua changamoto za wakulima kutofikia gharama za pembejeo na kuwasaidia
kujikamua katika uzalishaji kwa kuwa na pembejeo bora na kwa wakati,”alisema
Mkindi.
Kongamano
limeandaliwa na Jukwaa la Uchambuzi wa Sera za kilimo kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali wa Sekta binafsi na za umma ili kuleta mageuzi
katika sekta ya Kilimo na kuchangia katika ukuaji wa Viwanda na
kuhudhuriwa na takribani zaidi ya washiriki 300 nchini.
Post a Comment