Wabunge , Peter Lijualikali na Susan Kiwanga Wafikishwa Mahakamani
Wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) na Susan Kiwanga wa Mlimba na wenzao saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kukamatwa na polisi.
Kwa
mujibu wa Kaimu Katibu wa Vijana Chadema mkoa wa Morogoro, Jackson
Malisa, Wabunge hao walikamatwa Jumatano iliyopita ya Februari 20, 2019
wakiwa Kijiji cha Sofi wilaya ya Malinyi na kukaa rumande hadi leo
Jumatatu Februari 25, 2019.
Bado
haijafahamika wabunge hao na wenzao wana tuhuma gani, lakini wiki
iliyopita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa
alisema jeshi hilo lilikuwa linawasaka wabunge hao pamoja na wanachama
11 wa Chadema walioachiwa huru na mahakama mkoani humo Januari 2019.
Waliachiwa huru kupitia kifungu cha Sheria namba 225 cha mwenendo wa makosa ya jinai baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto ofisi ya Sekondari ya kijiji cha Sofi Wilaya ya Malinyi.
Mutafungwa alisema kuwa jeshi la Polisi hivi sasa wamejipanga kwa kuwa na ushahidi na vielelezo vya kutosha vya kuwatia hatiani watuhumiwa hao waliokuwa wameachiwa huru na Mahakama.

Post a Comment