SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUTEKELEZA MRADI WA UENDELEZAJI NA UPATIKANAJI WA MBEGU ZA MAZAO JAMII YA MIKUNDE NA NAFAKA AFRIKA (AVISA)
Mgeni
Rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza ushirikiano
wa serikali kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo wakati akifungua
mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii
ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount
Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi
ya washiriki wakifatilia mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji
wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika
katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Mgeni
Rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati
akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za
mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika
ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Daqarro akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa Mradi wa
uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka
Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini
Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Arusha
Serikali
imeeleza kuwa imejipanga kuweka mazingira wezeshi katika kutekeleza
Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde
na nafaka Afrika (The Accelerated Varietal Improvement and Seed Delivery of Legumes and Cereals in Africa project-AVISA).utakaosimamiwa na kutekelezwa kwa ukamilifu nchini Tanzania.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 25 Februari
2019 wakati akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa
mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika
katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha.
Katika
ufunguzi huo wa mkutano wa siku tatu, Mhe Hasunga alisema kuwa ana
mategemeo makubwa kuwa katika mradi huo msukumo mkubwa utawekwa katika
uhaulishaji wa teknolojia kupitia uimarishaji wa mashirikiano kati ya
sekta ya umma na sekta binafsi ili matokeo ya mradi yaweze kuonekana kwa
walengwa.
Alisema,
Kilimo kimeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi katika nchi nyingi za
Afrika ikiwemo Tanzania. “Kwa mfano, hapa Tanzania kilimo kinachangia
asilimia 29.1 katika pato la taifa na karibia asilimia 65.5 ya nguvu
kazi inategemea kilimo”
“Hata
hivyo, kwa Afrika kilimo kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni
pamoja na ukame, upungufu kwa rutuba katika udongo, kuongezeka kwa
magonjwa na wadudu wa mazao vipando, miundombinu hafifu, kipato kidogo
kwa wakulima, upokeaji mdogo wa teknolojia, soko lisilokuwa la uhakika
na bei ndogo za mazao, kutegemea kilimo cha jembe la kutumia mkono na
mifumo hafifu ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora. Hivyo, hali hii
inasababisha uzalishaji mdogo, ubora mdogo wa mazao na kuwafanya
wakulima kubakia kuwa wadogo na kulima kwa kujikimu tu sio kibiashara”
Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema
kuwa, ana matumaini makubwa kuwa Mradi huo utaimarisha mafanikio
yaliyopatikana kutoka kwenye miradi ya utafiti iliyotangulia ya Mikunde (Tropical
Legumes -TL), Uendelezaji wa Tija katika Mazao ya Mtama na Ulezi
(Harnessing Opportunities for Productivity Enhancement for Sorghum and
Millets - HOPE) na Harvest Plus ambayo ilifadhiliwa na Shirika la Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF) – kwa ajili ya kuendeleza uzalishaji wa mbegu na usambazaji wake.
Aidha, BMGF
imekuwa ikifadhili miradi hiyo katika nchi saba (7) za Afrika zikiwemo
Tanzania, Uganda, Ethiopia, Burkina Faso, Ghana, Mali na Nigeria katika
utafiti wa dengu, karanga,
maharagwe, kunde, mtama na ulezi. Hivyo, Mradi huo wa AVISA utaendeleza
na kuimarisha mashirikiano kati ya Vituo vya Kimataifa
vya Utafiti wa Kilimo (CGIAR) na Mifumo ya Kitaifa ya Utafiti wa Kilimo
katika nchi za Afrika (NARS) katika kuendeleza uzalishaji na usambazaji
wa mbegu za aina ya nafaka na mikunde zinazohimili maeneo ya ikologia
ya ukame.
Manufaa
mengine ni kuimarisha na kuongeza madini ya chuma na zinki katika mazao
ya maharagwe na ulezi katika mradi wa HarvestPlus unaofadhiliwa na BMGF
kupitia CIAT (Maharage) na ICRISAT (Ulezi). Hivyo, kuwekeza Miradi
miwili ya TL-III na HOPE ambapo itaongeza tija kwenye mazao husika na kujenga uwezo wa utafiti kwenye nchi zetu za Afrika.
Post a Comment