VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA
Mwambawahabari

WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana mkoani Kigoma waanzishe mashamba
ya michikichi kwa kuwa zao hilo litawapatia kipato cha uhakika.
Amesema
Serikari imedhamiria kufufua zao la michikichi ili kuliwezesha Taifa
kujitosheleza kwenye mafuta ya kula na kuokoa fedha za kigeni.
Ameyasema
hayo leo (Jumatatu, Februari 18, 2019) alipowasalimia wananchi wa
kijiji cha Nyakitondo wilayani Kasulu akiwa njiani kwenda Kibondo.
Waziri
Mkuu ambaye yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi yenye lengo la
kufufua kilimo cha michikichi amesema ni vema wananchi wakachangamkia
fursa hiyo.
“Vijana
limeni michikichi kwani ukipanda ukiwa darasa la tano baada ya miaka
mitatu utaanza kuvuna na kujipatia kipato ambacho kitakuwezesha
kujikimu.”
Amesema
kilimo cha zao la michikichi kitawawezesha wananchi hususani vijana
kupata mitaji ya uhakika kwa ajili ya shughuli zingine za kiuchumi
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania
inaongoza kwa kilimo cha zao la michikichi katika nchi za Afrika
Mashariki.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi hao wajiunge na Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) ili wawe na uhakika wa matibabu kwa yao na familia zao.
Wakati
huohuo Waziri Mkuu ametembelea kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani
Kibondo na kukagua shule ya msingi Kassim Majaliwa na baadae wodi ya
wazazi katika Hospitali Nduta.
Post a Comment