SERIKALI YALAANI MAUAJI YA WATOTO
Mwambawahabari
Na WAMJW – DSM
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amelaani mauaji na matendo ya kikatili yote
yanayofanywa dhidi ya Watoto, huku akivishukuru vyombo vya Dola kwa hatua za
haraka wanazoendelea kuchukua katika kudhibiti matukio hayo.
Ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya
Makazi ya Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar
es salaam.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali haiwezi kuvumikia mambo
yakikatili yanayofanywa dhidi ya Watoto na haki zao, hivyo itawachukulia hatua
yeyote atakae bainika amekwenda kinyume na kuvunja sheria zinazomlinda mtoto.
"Tunalaani sana, mauaji haya ya Watoto, na tunavishukuru
vyombo vya Dola vimeweza kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kwamba
vinadhibiti matukio haya" alisema Dkt. Ndugulile
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa Waganga wote wa Tiba
Asili na Tiba Mbadala kuacha kutumia viungo wala miili ya Watoto kama njia
yakutatua matatizo kwa wateja wao, hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa watakao
kaidi agizo hilo.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Waganga wa Tiba Asili na
Tiba mbadala wote ni lazima wahakikishe wanajisajili katika Mamlaka na Baraza
husika ili kuepuka usumbufu na hatua kali dhidi yao pindi watakapobainika hawajafanya
hivyo.
Ameongea kuwa Waganga wa Jadi watakaobainika na kujihusisha na shughuli zisizosajiliwa katika shughuli za Tiba
Asili na Tiba Mbadala watachukuliwa hatua kali sana za kisheria dhidi yao na hata wale ambao watajihusisha pamoja na waganga hao.
Dkt. Ndugulile pia ameutaka Uongozi wa Makazi ya watoto waishio katika mazingira magumu kuwajibika katika
baadhi ya mambo ikiwemo masuala ya usafi wa mazingira , Mabweni na mavazi kwa
watoto uzingatiwe na kuaagiza kuweka magodoro mapya, mashuka na chandarua katika mabweni hayo.
Naye Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bi. Beatrice Mgumiro amesema kuwa makazi hayo
yanajumla ya watoto 70 ambapo watoto 54 wapo katika makazi hayo na watoto 16
wapo wanasoma katika shule za bweni.
Bi. Beatrice amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa atatekeleza maagizo
yote aliyompa na ameishukuru Serikali kwa uangalizi wa karibu wa watoto waishio
katika mazingira magumu kwa kutoa huduma muhimu kwa watoto hao ikiwemo malazi
chakula na elimu.
Post a Comment