Waziri Wa Kilimo Akutana Na Rais Wa Shirikisho La Vyama Vya Ushirika Duniani

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Jana tarehe 21 Januari 2019 katika
ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu (Kilimo I) Mtaa wa Tazara Jijini Dar
es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la vyama
vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco.
Katika
mkutano huo uliotanguliwa na ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
vyama vya Ushirika Jijini Dar es salaam Rais huyo ameambatana Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho hilo Ndg Bruno Roelants pamoja na Rais wa
Shirikisho la vyama vya Ushirika Afrika Ndg Japhet Magomere na Katibu
Mkuu wa Shirikisho la hilo barani Afrika Bi Chiyoge Sifa
Pamoja
na mambo mengine Mhe Hasunga amemuhakikishia kiongozi hugyo wa
Shirikisho hilo kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais
Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha mapungufu ya muda mrefu
kwenye vyama vya Ushirika ikiwemo kushughulikia viongozi wabadhilifu.
Hasunga
alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya
sifa za viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini ili kupata viongozi
watakao ongoza kwa weledi sekta ya Ushirika.
Alimueleza
Rais huyo kuwa Dhana ya kuchagua viongozi wa ushirika wenye sifa ya
kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati hivyo kuna kila sababu ya
kuchagua viongozi wenye weledi na utashi katika utendaji.
Aliongeza
kuwa mfumo wa ushirika ni nyenzo muhimu ambayo ukitumika vizuri
itasaidia kuondoa umaskini wa wakulima hapa nchini na Dunia kote
utaimarisha uanzishwaji wa viwanda kuleta tija katika kilimo hivyo ni
lazima kuwa na juhudi za makusudi kuwa na viongozi wenye weledi.
Alisema
kuwa Wizara yake pia imeanza kupitia upya sheria ya vyama vya Ushirika
ili kuwa na Ushirika imara na wenye nguvu na tija kwa wakulima kwani
kufanya hivyo kutaongeza Imani ya wananchi waliokata tamaa na Ushirika.
Alisema
pia miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya Ushirika nchini ni
kukosekana kwa taarifa sahihi za wanachama (Data Base) kuanzia vyama vya
msingi (Union) hadi vyama Vikuu vya Ushirika (AMCOS) jambo ambalo kwa
muda mrefu limepelekea kuwa na Ushirika usiokuwa na tija na manufaa kwa
wakulima wanaotumia nguvu na rasilimali zao nyingi katika kilimo.
Naye,
Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco
amesema kuwa msingi wa ziara yake hiyo katika Afrika Mashariki pamoja
na nchi zingine ni sehemu ya utekelezaji wa wajibu wake ambapo alianzia
Kenya, Rwanda na sasa Tanzania.
Alisema
kuwa Tanzania ni miongoni kwa nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara
ambayo imepokea vyema dhana ya Ushirika ambapo serikali inaunga mkono
kwa kiasi kikubwa hivyo ana Imani miaka michache ijayo kupitia mfumo huo
wakulima watakuwa na mafanikio yasiyopimika.
Alisema
kuwa amezuru nchini Tanzania kwa ajili ya kuonana na kufanya mazungumzo
na wana Ushirika ikiwa ni sehemu ya kubaini na kuzitafutia ufumbuzi wa
haraka changamoto mbalimbali kwenye sekta ya Ushirika. Vilevile ameeleza
kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano uliyopo
baina ya Tanzania na Shirikisho hilo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la vyama vya Ushirika
Tanzania (TFC) Bi Aberhad Mbepera alisema kuwa ziara ya Rais huyo ni
sehemu ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na ICA.
Alitoa
wito kwa wakulima kujiunga na vyama vya Ushirika kwani katika Ushirika
kutaimarisha umoja na mshikamano kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na
kauli moja katika kupanga bei ya bidhaa zao pasina kugalalizwa.
Akitoa
neno la shukrani Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt
Titus Kamani alisema kuwa maisha ya watanzania yataimarika kupitia
Ushirika hivyo Tume hiyo imejipanga kutoa elimu kwa wakulima nchini
kuelewa umuhimu wa kujiunga na mfumo wa Ushirika.
Alisema
Ushirika ni nyenzo pana katika maisha halisi ya wananchi kwani hatua
mbalimbali za wananchi zinategemea Ushirika kuanzia maisha ya kawaida,
biashara na kilimo.
Aliongeza
kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika imedhamiria kuwanufaisha watu
masikini kuwa na kipato cha kati kitakachomudu ukali wa maisha na kuwa
na utajiri.
Post a Comment