WAISLAM DAR WAADDHIMISHA MAULIDI YA MAZAZI YA MTUME MUHAMADI ( S.A.W) .
Kiongozi mkuu wa dini Al Allahmah Al Habibu Umar Bin Muhammad Bin Salim Bin Hafidh, akiteta jambo na badhi ya viongozi na waumini wa dini ya kiislam walioudhuria hafla ya Maulid ya Mazazi ya Mtume Mohammad (S.W.A) iliyoa andaliwa na Uongozi was kampuni ya Nida textiles na Namera Group LTD
Waumini wa Dini ya kiislam nchini, wamefanya hafla ya Maulid ya Kuadhimisha Mazazi ya Mtume Mohamed (S.A.W). Iliyoandaliwa na kampuni ya Nida textile na Namera Group (LTD) .
Waziri wa ulinzi na Usalama nchini Mhe. Hussein Mwinyi akizungumza Katika hafla hiyo, amewataka waislam kote nchini kudumisha amani na Umoja kwani amani Ndio mwanzo wa Kila kitu.
Amesema Umoja uliopo miongoni mwa waislamu uendelee kudumu,kwani kukiwa na amani na nchi pia inakuwa ya amani Kama ilivyo Sasa
Aidha Amesema kufuata mafundisho ya dini Pamoja na kuendelea kushinana ili kuendelea kusogeza mbele maendeleo ya nchi.
Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam imehudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Al Hassan mwinyi, Waziri wa Ulinzi, Dkt Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mifugo, Abadllah Ulega, Mufti Mkuu wa Tanzania,
Aboubakary Zubery, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Bin Zubery, Masheikh wakuu wa mikoa mbalimbali pamoja na wageni kutoka nje ya nchi.



Post a Comment