SAKATA LA NDUGAI CAG LATUA LHRC,WATOA UFAFANUZI Kisheria Kuhusu Mamlaka na Mipaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali-CAG

Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali ni ofisi ambayo imeundwa kikatiba kupitia Ibara ya 143 na 144 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara.
Ibara hiyo kwa ufupi inaeleza ifuatavyo;
143.-(1)
Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri
ya Muungano.(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na jukumu juu
ya mambo yafuatayo:
(a)
kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko
Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba
zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya Katiba hii, na
iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi
ataidhinisha fedha hizo zitolewe;
(b)
kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa
yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au
fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na
Bunge, na ambazo zimetumika, zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo
husika na matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo yamefanywa kwa
kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo; na
(c)
angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya
ukaguzi wa hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabu
zinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
hesabu za Mahakama zote za Jamhuri ya Muungano na hesabu zinazosimamiwa
na Katibu wa Bunge.
(3)
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na kila mtumishi wa Serikali
aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na haki ya
kuchunguza vitabu, kumbukumbu, hati nyinginezo zote zinazohusika na
hesabu za aina yoyote iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais
kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya
ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu
wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge
kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi
iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile
kilipoanza kikao hicho.
Iwapo
Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge
(au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi wakati huo au ikiwa kwa
sababu yoyote Spika hawezi kutekeleza shughuli za kazi yake) ambaye
atawasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge.
(5)
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia na jukumu la kutekeleza
kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na madaraka mengine ya namna
mbalimbali, kama itakavyoelezwa na sheria kuhusu hesabu za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano au hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za Mashirika.
(6)
Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote
au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo
hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza
kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.
Uwajibikaji/Kuwajibishwa kwake
1.Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anawajibika kwa Rais sio kwa
Bunge. Ibara ya 143 (4). Bungeni huwasilisha taarifa ambayo imetoka kwa
Rais.
ii.Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikai halazimiki kufuata Maagizo ya mtu yeyote Ibara ya 143 (6).
iii.Mahakama
ina uwezo wa kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii ama
sivyo.Ibara ya 143 (6).
iv.Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataondoka kazinikwa yafuatayo;
a)Kustaafu
b)Kuugua
c)kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. lbaya ya 144
Post a Comment