Ads

NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA : WATOTO YATIMA NI WATOTO WETU TWAPATIENI MSAADA



Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu  Stella Ikupa ,akimkabidhi  Beatrice  Laurence ,Afisa ustawi wa Jamii,Baadhi ya vitu alivyo toa msaada katika  makao ya watoto yatima kurasini,aliye upande wa kushoto ni Mbunge wa viti maalumu Temeke, Mariam Kisangi.(Picha zote na John Luhende)




Na John Luhende
Watanzania  wameaswa kujitoa kwa  hali na mali katika kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika vituovya kulelea watoto kwani wanayo mahitaji kama walivyo wengine wanaoishi majumbani na familia zao, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuugusa  moyo wa Mungu moja kwa moja .

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu  Stella Ikupa  , alipo tembelea  na kutoa msaada  katika Makao ya Watoto yatima Kurasini ,ambapo ametoa rai kwa  watanzani kuendelea kujitoa wanapo pata nafasi kutembelea na kutoa misaada kwa watoto hao.

“Hawa ni watoto wetu tuendelee kujitoa tunakaamajumbani kwetu tunakula na kusaza tunamwaga vyakula kumbe kuna mtoto ambaye amelala njaa kwa sababu hana mzazi wa kumhudumia ,  kwahiyo nijambo jema tukitumia kidogo tunachokipata kugawana na wengine,hata Maandiko matakatifu  yanasema, Dini iliyonjema  ni kuwaona yatima na wajane katika shida zao na mtu anapofanya hivi anamgusa Mungu”Alisema 

Aidha Mhe. Ikupa ameushukuru uongozi ya Makao ya watoto hao  kwa kuendelea kuwalea vizuri  watoto hao na kuupongeza uongozi wa CCM kutoka Umoja wa wanawake (UWT) ambao nao waliambatana naye katika kutoa msaada huo pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mariam Kisangi .
Kwa upande wake Afisa ustawi  aliyemwakilisha Kamishina wa Ustawi  wajamii ,Kutoka wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto,katika hafla hiyo Rehema Kombe ,amemshukuru  mhe. Stella Ikupa, kwa moyo wake wa upendo na kuona umuhimu wa kuwasaidia  na kutoa huduma kwa yatima  na kusema kuwa watoto hao ni watanzania na wanamahitaji wanayo yahitaji kama wengine  na kutoa wito kwa viongozi wengine  kuwa na moyo huo .

“Watoto hawa wamekosa wazazi wanahitaji ada za shule ,mavazi , chakula ,malazi na mengine yaliyo mahitaji ya kibinadamu , tunapokuwa tunasherehekea tunafurahi huko majumbani tuwakumbuke nawatoto hawa ,niwaombe sana viongozi , mashirika ,taasisi na watanzania kwa ujumla tuwajali niwatoto wetu sote kutoa nimoyo ukitoa kidogo ulicho nacho Mungu anakubariki” Alisema 

Wakitoa neno la shukrani watumishi na baadhi ya watoto, wameshukuru  kwa kuwajali na kuwathamini  pia  wamesema wataendelea kumuombe kwa Mungu Mhe.Ikupa  ili amuongezee palipo pungua na kumfungulia Baraka .

Mariam Kisangi ambaye ni Mbunge viti Maalumu  Temeke , Mkoa wa Dar es salaam,akizungumza Makaoni hapo, amewapongeza na kuwatiamoyo walezi na wafanyakazi wa kituo  hicho na kuwaambia kuwa kazi wanayofanya ni kazi ya wito nikama kazi ya mungu na fungu lao kubwa liko kwa Mungu  ,huku akipongeza serikali kwa maboresho ya kituo hicho kwani kipindi cha nyuma hakikuwa hivyo.

“Nawaomba watoto wetu mpendane na muwapende walezi wenu na walimu wenu ili muendelee na masomo”Alisema


Baadhi ya vitu vilivyo tolewa ni pamoja na ,mchele, Unga wa Ngano na sembe, ,Sabuni ya unga , miche,Matunda Madaftari kalamu,Sukari ,Mikate,Biscuits, Katoni za Juice,Mafuta ya kupikia na Taulo za kike.








No comments