MAMA MLEMAVU ALIYESAIDIWA BAJAJI NAIBU WAZIRI STELLAIKUPA, ANENA MAZITO .
Na. John
Luhende
Mwamba wa Habari
Mwamba wa Habari
Wito
umetolewa kwa wadau binafsi ,Makampuni na Mashirika mbalimbali kuwasaidia watu
wenyeulemavu ,ili kukidhi mahitaji yao ikiwemo kuwaendeleza katika shughuli na
vipaji vyao.
Witohuo
umetolewa na Naibu Waziri ,Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu Stella
Ikupa,alipokuwa akikabidhi Bajaji kwa Mama Leonea Leonard ambaye ni mlemavu
wa miguu ,ambapo amesema Bajaji hiyo ameipata kwakushirikiana na mdau baada ya
kumweleza kuhusu shida ya Mama huyo.
“Wahitaji wako wengi Tanzania
,unawezakumsaidia Mama leonia au unaweza kumsaidia mhitaji mwingine ,leo
tumempatia Bajaji inaweza kumsaidia katika shughulizake lakini pia bado analo
hitaji lakusaidiwa kurecord nyimbo zake
,tunaomba mdau mwingine aweze kujitokeza amsaidie aweze kurecord
‘’Alisema
Kwaupande wake Mama Leonea Leonard ,amemshukuru Mhe. Stella Ikupa, kwa moyo wake wa kujali watu bila kujali kuwa
ni ndugu yake ama kuwa anaulemavu bali anasaidia watu wote ,amesema watu wengi
wanauwezo kifedha lakini hawana moyo wa
kusaidia ,Bajaji hii angeweza kuitumia kwa mambo yake mengine lakini kaamuamua kumpatia yeye hivyo
amemshukuru Mungu kwa Upendo huo.
‘’Stella Ikupa
,Joshua na Mkewake kwapamoja nawashukuru sana Mungu awabariki
,Kwa nisaidia Bajaji hii sina cha kusema sana zaidi ya kuwashukuru na kuwaombea
Mungu awainue mzidi kufanikiwa ,Bajaji hiimimi itanisaidia sana sina mahali pa
kuishi naweza kukusanya kidokidogo nami niwe na makazi yangu na pia nahitaji sana kurecord nyimbo
zangu”Alisema.
Post a Comment