KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI (TIC) CHAFURAHISHWA NA HATUA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI, KWA KUWAPA WIZARA KAMILI.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezajiji (TIC) Geofrey Mwambe, akizungumza na waandishi
wahabari (hawapo pchani) pamoja na maafisa wa kituo hicho leo jijini Dar es slaam( Picha na
John Luhende).
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezajiji (TIC) Geofrey Mwambe, akizungumza na waandishi
wahabari pamoja na maafisa wa kituo hicho leo jijini Dar es slaam( Picha na
John Luhende).
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT John Magufuli kwa kufanya maamuzi ya kuanzisha Wizara inayoshughulikia masuala ya uwekezaji, tofauti na awali ambapo shughuli zote za TIC zilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa. Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuona umuhimu wa kukihamishia Kituo hicho ofisi ya Waziri Mkuu, kwani kitarahisisha utekeleji wa majukumuyake ikiwemo kusukuma haraka juhudi za uanzishwaji wa Viwanda
nchini.
Ameongeza kuwa, TIC ni muhimu
kwa kujenga uchumi wanchi na kwamba kitendo cha kituo hicho kupewa Waziri wake
na Katibu mkuu wake utaharakisha na kurahisisha utekelezaji wa mipango yake,hivi karibuni Rais Magufuli, alimteua Mhe. Angellah Kairuki, kuwa waziri wa Uwekezaji na Doroth Mwaluko, kuwa
katibu mkuu.
Aidha ametoa wito kwa taasisi binafsi, taasisi za Serikali pamoja na serikali za mitaa, kushirikiana na TIC katika kutangaza fursa za uwekezaji ndani na nje ya nchi.
"Jana nimeongea sana na Waziri
wa Fedha, amesisitiza tujitahidi sana kujenga mazingira ya uwekezaji na yawe
rafiki zaidi asiwepo mtu wa kukwepa kulipa kodi na tukifanya hayo tutamsaidia
sana Rais na wawekezaji waendelee kuiona Tanzania kuwa nchi salama katika
Uwekezaji "Alisema Mwambe.
Hata hivyo amezitaka taasisi binafsi
na mashirika yasiyo ya kiserikali, kushiriki kikamilifu katika kutangaza fursa za uwekezaji na kusema kuwa hali ya uwekezaji Duniani mwaka 2018, ilishuka kwa 23% kwa Afrika Mashariki Tanzania ilipata Dola za kimarekani billion 1.365 mwakaka 2017,mwaka 2018 ilishuka hadi dola za kimarekani billion 1.2
lakini iliongoza Afrika Mashariki
na kufanya vizuri kimataifa.
" Nimeona clip ya Tundu Lissu
alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni huko nje ya nchi, huo siyo uzalendo
inaonekana Mtangazaji anajua zaidi anaipenda Tanzania kuliko yeye,
nimemshangaa sana ,anaibomoa nchi wakati
yeye ndiyo anasema anataka kugombea 2020"alisema.
Watanzania wanalo jukumu kubwa kuisemea
vizuri nchi yao kimataifa na kwamba inaongoza kuwa na mazingira Mazuri ya
uwekezaji na haina tishio lolote la kigaidi kama iliyo kwa nchi nyingine.
"Naomba sana wanahabari na
watanzania wote tushirikiane na Tundu Lissu naye ni mtanzania namuomba aache kuichafua
nchi maana mwisho wa siku atarejea hapanchini, namimi nita ongea
naye, anatakiwa kuwa balozi wa Uwekezaji huko aliko" Alisema.
Pamoja na hayo Mwambe ameishukuru
Serikali kwa kuiongezea watumishi wa TIC na Mikoa iliyotenga maeneo ya
Uwekezaji.
"Naishukuru Mikoa ambayo
imetenga maeneo ya uwekezaji na kuyapima hiyo itatusaidia kwa wawekezaji wapya" Alisema.
Akijibu swali kuhusu wawekezaji wa kubwa amesema, Mradi wa kiwanda cha Cement hengya Tanga ni moja ya miradi mikubwa na unaendelea
vizuri, katika eneo la mtimbwani Mkinga, kitakuwa kinatengeneza Cement
marambili ya kiwanda cha Dangote cha Mtwara, kitakuwa na bandari yake kwaajili ya
usafirishaji mizigo.


Post a Comment