Katibu Mkuu Wa CCM Dkt. Bashiru Ally Atembelea Kaburi La Baba Wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera
Katibu
Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally atafanya ziara ya siku mbili kuimarisha
Chama Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama
alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere
Aidha,
Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama
nakukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere
Ndg.
Bashiru Ally ameyasema hayo Mbele ya wananchi na viongozi wa Chama na
serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Ndg. Samweli Kiboye
wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda
Katika ziara hiyo ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Butiama.
Katika
kikao hicho Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. John Pombe Magufuli kwa wana Mara
na kuwambia anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo,
ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma
itatekelezwa.
Post a Comment