WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKULIMA WA KOROSHO
Mwambawahabari
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kiwanda
cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti (wapili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti (wapili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa
Mathias wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza
baada ya kutembelea kiwanda hicho, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
.....................................................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa.
Amesema
Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na
hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa
kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama
kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.
Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika.
Waziri
Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara
kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
“Lengo
la Serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais Dkt. John
Magufuli alisitisha ununuzi baada ya kuona wakulima wanataka
kudhulumiwa.”
Waziri
Mkuu amesema kuwa hadi sasa tayari tani 181,000 zimeshakusanywa, hivyo
amewataka wakulima wa zao hilo nchini waendelee kuiamini Serikali yao.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono
jitihada za Serikali kukuza uchumi kwa kupitia sekta viwanda.
Awali,
Meneja Utawala wa kiwanda cha Terra, Peter Ngwale alisema uwezo wao ni
kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tano 3,000.
Pia
aliiomba Serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa
kiwango cha ubora kinachoandikwa kinakuwa tofauti na uhalisia wa
korosho yenyewe.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, DESEMBA7, 2018.
Post a Comment