SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO WADAU WA HAKI YA AFYA YA UZAZI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM CHINI YA TGNP MTANDAO
TGNP Mtandao kwa kushirikiana na shirika
la Afrika Kusini la (Gender Links) wamekutanisha wadau mbalimbali wanaofanya
kazi katika eneo la Afya ya Uzazi lengo likiwa ni kujadili changamoto
zinazoikabili sekta hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mapema
jana jijini Dar es salaam na Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja
wa TGNP Bi. Anna Sangai alisema kuwa wameamua kufanya mkutano huo ikiwa ni
miongoni mwa sehemu ya kuendelea kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia.
Aliendelea kusema kuwa malengo mengine
ni kujitathmini kwa kina walipotoka, walipo na wanapoelekea katika swala la
ukatili wa kijinsia pamoja na kuangalia kama taifa linaendana na mikataba
mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo nchi yetu imekubali kuingia na
kuitekeleza.
Aidha ameongeza kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa wakipata
changamoto mbalimbali katika shule nyingi ikiwemo mazingira wezeshi kama vyumba
vya kujihifadhia, ukosefu wa maji na hata baadhi ya shule hazina milango ya
vyoo hali inayompa ugumu mtoto huyo.
"Shule nyingi kwa sasa zimekua hazina mazingira rafiki kwa
wananfunzi wa kike, hivyo kupelekea kukumbana na changamoto mbalimbali, lakini
mkutano huu utaangalia makubalino ya kikanda na kimataifa ambayo
yamelenga kuwepo kwa haki ya kijinsia "amesema Anna.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taatisi ya Center
Against Gender Violence (CAGBV) Sophia Komba amesema haki ya afya ya
uzazi na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa katika afya ya uzazi bado ni
changamoto kubwa sana nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa, mkutano
huo utajadili namna gani ya kuweza kukabiliana na changamoto za afya ya uzazi
na kuweza kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia
ili kuwepo kwa usawa na upatikanaji wa huduma ya afya ya uzazi..
Aidha ameiomba Serikali kuweka sera madhubuti pamoja na
kutekeleza mikataba mbalimbali ya kimataifa ya za huduma ya uzazi wa mpango na vijana hali
itakayochangia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na nyanyasaji.
Mshauri wa shirika la Gender Link lenye Makao Makuu yake nchini Afrika ya Kusini Bi. Kubi Rama akitoa ufafanuzi wa jambo mapema jana katika ufunguzi wa Semina inayohusu maswala ya Afya ya Uzazi.
Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taatisi ya Center Against Gender Violence (CAGBV) Bi. Sophia Komba akichangia mada katika semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Post a Comment