RC Kilimanjaro Aagiza Ng'ombe Waliovamilia Mashamba Ekari 4 Wapigwe Mnada Kufidia Uharibifu Huo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, ameagiza kukamatwa na kupigwa mnada kundi la mifugo inayodaiwa kuvamia mashamba ya wakulima katika kijiji cha Chemchem, Wilaya ya Moshi, baada ya kuharibu zaidi ya ekari 400 za mazao ya chakula.
Dk.
Mghwira ametoa agizo hilo jana katika salamu zake za sikukuu za
krismasi na mwaka mpya, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
mkoa ulivyojipanga kuimarisha ulinzi kila kona.
“Nimeshaagiza
vyombo vyetu vya usalama kwa maana ya Jeshi la Polisi likamate mifugo
ya wafugaji ambayo ilikula mazao ya wakulima wa kijiji cha chemchem na
ipigwe mnada ili fedha zitakazopatikana ziwafidie wakulima waliopata
hasara ya kupoteza mazao yao.
“Pia
nimewaagiza Wakuu wa Wilaya za Moshi na Mwanga wasimamie utekelezaji wa
agizo hili. Hatuwezi kaucha mchezo huu ukaendelea kila mwaka, lazima
kuwe na heshima dhidi ya dola.”
Siku
nne zilizopita, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Kadiria Mmari, alitoa
taarifa kuwa moja ya mazao yaliyoharibiwa vibaya ni pamoja na mahindi,
nyanya, kabichi, bamia na tikitiki maji.
Mifugo
kutoka Wilaya hiyo ya Simanjiro imekuwa ikifanya uharibifu mkubwa wa
mazao yao kwa miaka minane mfululizo, bila kupatiwa ufumbuzi.
Mifugo hiyo inadaiwa kutokea vijiji vya Magadini, Kiruwani, Msitu wa Tembo na kambi ya chokaa vilivyopo mkoa wa Manyara.
Mifugo hiyo inadaiwa kutokea vijiji vya Magadini, Kiruwani, Msitu wa Tembo na kambi ya chokaa vilivyopo mkoa wa Manyara.
Post a Comment