NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII.
Naibu Meya
wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi Mchele kwa kikundi cha
akinaMama wajane wa kata ya Vingunguti (Picha zote na John Luhende)
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Akina
Mama wajane katika kata ya vingunguti wametakiwa kuwa na umoja ili kuwa kukabili
changamoto za maisha zinazowakabili na kuweza kupata msaada wa kijamii kutoka
serikalini na wafadhili mbalimbali na
watu binafsi .
Wito huo
umetolewa na Naibu meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Vingumguti Omary Kumbilamoto, alipokuwa akitoa msaada wa vyakula kwaajili ya
sikuu ya Christmas kwa kikundi cha Upendo cha akinamama wajane kata ya Vinguti
, na kuitaka jamii kutoyasahau makundi ya wajane yatima na walemavu.
‘’Akina Mama
hawa hawakuwa na pakushika sikukuu hii, ni likutana nao siku tatu zilizopita wakaniomba nikawaahidi kuwa saidia, na leo
nimewaletea Mchele kilo 100,na Mafuta ndoo moja , kubwa zaidi
nina sisitiza wawe na umoja ili iwe rahisi kuwa fikia na kuwapa msaada,namimi
nimefanya mengi katika kata hii ikiwemo kununua gari la wagnjwa katika zahanati
ya Vingunguti, nitawasaidia kuwa tafutia wadu na pia nitamleta afisa Maendeleo
ili awape elimu na wafungue account “alisema
Aidha
Kumbilamoto ameitaka jamii kuwa na huruma kwa wajane kutowanyang’anya mali walizo achiwa na waumezao.
“Naomba
jamii tuyaangalie haya makundi maalum ya Walemavu wajane na Yatima ,pia
sibusara sana kwa wanajamii kunnyang’anya maliza za malehemu wajane wanateseka na yatima, kwa hapa Vingunguti tuna viwanda
41, nita waomba nao wasaidie kundi hili “alisema
Kwa upande
wake mwalimmu wa kikundi hicho Jane
Raulent, amesema amefanikiwa kuwaweka
pamoja wajane hao na sasa wana saidiana
kuweza kupata chakula kwa kuchangia fedha kidogo.
‘’Nimejaribu
kuwa saidia kwa kuwaweka pamoja hapa mwanzo walikuwa wanateseka walikuwa
wanaokota vikuni na vifuu barabarani na chakula ilikuwa shida kwa sasa
wanachangiana chakula kwa kuto shilingi
elfu tano kila mjane anapata kiroba kimoja cha unga , na muda mwingine mafuta ya taa
na mkaa”alisema
Nao baa dhi
ya akimama wajane waliopatafursa ya kuzungumza wamemshukuru Naibu Meye
Kumbilamoto kwa msaada aliowapa na kumuoma awatafutie wafadili wa kikundi hicho.
“Jinalangu
naitwa Mariam Daud Hashim,ni mjane
nifiwa na Mume wangu 2007, haijawahitokea kwa viongozi hatawaliopita sikuwahi kuwaona
wakisaidia wajane hadi mimi leo nimetimiza miaka 70, naona viongozi waliowengi wanajali familia zao na
wanajilimbikizia mali , tunakushukuru wewe Baba kwa moyo wakutoa Mwenyezi Mungu
akuzidishie ulipotoa ’’alisema.













Post a Comment