MHE HASUNGA AITAKA TFC KUSHIRIKIANA NA NJORECU KUHARAKISHA UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA
Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga (Mb) Mwenye Tai, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji hao Jijini Dar es salaam, leo tarehe 11 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China, leo tarehe 11 Disemba 2018 Jijini Dar es salaam.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Mwamba wa habari
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza Shirikisho la vyama vya ushirika
Tanzania (TFC) kushirikiana vyema na Chama Kikuu cha Ushirika Njombe (NJORECU)
kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea unaanza mapema kabla ya
mwezi June mwaka 2019.
Alisema
kuwa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea utakapokamilika utawanufaisha wanaushirika wa
chama hicho cha NJORECU sambamba na wakulima wote nchini kwani kitaongeza
urahisi wa upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuzalishwa
hapa nchni.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 11 Disemba 2018
Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha
Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC)
pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China.
Mhe
Hasunga aliwashauri kuandaa andiko la mradi huo litakaloeleza aina ya mbolea
itakayozalishwa na taarifa zote zinazohitajika katika kufanikisha mradi huo
kuanza.
Wawekezaji
hao kutoka nchini China kwa kushirikiana na chama kikuu cha Ushirika Njombe
(NJORECU) wanataka kuwekeza katika ujenzi wa Kiwanda cha mbolea na kiwanda cha
kufungasha Viuatilifu vinavyotumika katika mazao ya Kilimo.
Katika
kikao hicho walieleza kuwa wawekezaji hao wapo tayari kuchangia asilimia 40% na
NJORECU (kwa maana ya Tanzania) asilimia 60% katika ukamilifu wa ujenzi wa
kiwanda hicho.
Kutokana
na umuhimu na uhitaji wa Mbolea nchini mjumbe wa bodi ya NJORECU alimweleza Mhe
Waziri wa Kilimo kuwa wamekwishapeleka maombi ya kuomba kushirikiana na NSSF
katika uwekezaji huo na wanasubiri majibu.
Wakati
huo hu, Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na
watendaji wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI).
Lengo
la mkutano huo ilikuwa ni watendaji wakuu hao kujitambulisha na kumueleza
Waziri wa kilimo shughuli wanazozifanya ili kuongeza ufanisi katika ushirikiano
na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BNI
ni muungano wa makampuni 8 yanayowahusisha wafanyabiashara kati ya 30 Duniani.
Post a Comment