Ads

DC Ilala atekeleza agizo la Rais agawa vitamburisho kwa wamachinga





Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akigawa kitambusho cha ujasiliamali kwa mmoja wa wafanyabiashara  wa Wilani Ilala , ambapo zoezi la kugawa vitambulisho hivyo limefanyika katika ofisi za wamachinga  kariako  na Ukumbi wa Anatougrom mnazi mmoja  mapema leo(Picha zote na John Luhende)




Na Heri Shaban
MKUU wa  Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amekabidhi vitamburisho vya wafanyabiashara wamachinga Kariakoo Dar es Salam.

Mjema amegawa vitamburisho hivyo  Dar es Salam leo siku moja baada agizo la Rais John Magufuli kuwagiza wafanyabiashara  wote watambulike wakiwa na vitamburisho hivyo vinavyotolewa vya Wajasiliamali wadogo.

"Katika Wilaya yangu  ya Ilala Leo nimegawa  vitamburisho 5000 kwa Wamachinga wa Kariakoo  ambao tulikuwa tunawatambua katika mfumo maalum, zoezi hili baadae litamia kwa   Mama ntilie wote waliopo Wilayani Ilala ambao mtaji wao chini ya shilingi milioni 4" alisema Mjema


Mjema alisema  Jumla 6233 Kati yake Wanawake 1225 wanaume 5000  wote watafanyabiashara zao bila kubuguziwa kama Rais alivyoagiza.

Alisema katika wilaya ya Ilala zoezi limekwenda vizuri  wamachinga walishawekwa pamoja katika Mfumo maalum ambao wanatambulika  rasmi na Serikali.

Aliwataka Wamachinga   na wafanyabiashara wote kufuata utaratibu    na wote watapewa vitamburisho  hivyo katika ofisi za Halmashauri jengo la Anatogluo.

Aidha alisema wote waliopewa vitamburisho wanatambulika na biashara Zao na Maeneo kama sio mfanyabishara uwezi kupewa KITAMBURISHO hicho.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa  Manispaa ya Ilala Elzabeth Thomas alisema Manispaa ya Ilala kama Halmashauri tumejipanga vizuri katika juhudi za kumsaidia Rais na Leo tumeanza na Wamachinga wa Kariakoo wote.

Thomas alisema Mpango huo wa kugawa vitamburisho ni endelevu mpaka wote wapewe vitamburusho Watendaji wake wa MANISPAA ILALA wanasimamia.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Kariakoo Yusuph Namoto alisema wao ni wazalendo  wanaungana na Serikali yao tukufu katika juhudi za kumsaidia Rais katika kukuza uchumi.

Yusuph alisema kwa sasa wanaitaji kukuza uchumi biashara zao kila wakati zinabadilika  hivyo wanaitaji uwezeshaji ili waweze kupiga hatua.





No comments