MABARAZA YA VIJANA VYAMA VYA SIASA YAPINGA MSWAADA WA VYAMAVYA SIASA ,YAAHIDI KUUCHANA.
Baadhi ya vijana kutoka Mabaraza ya vijana ya
vyama vya siasa wakishikana mikono kwa ishara ya mshikamanobaada ya
kusaini makubaliano ya ushirikiano katika kupinga mswaada wa vyama vya siasa
leo katika makao makuu ya NCCR MAGEUZI Dar es salaam (Picha na John Luhende)
Mabaraza ya vijana ya vyama vya Siasa nchini yameungana
katika kupinga mswaada wa vyama vya sia kwa madai kuwa unakandamiza vyama vya
siasa na kuhatarisha amani ya nchi.
Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini
Dar es salaam vijana hao wametishia kuuchana muswada huo pindi utakapofikishwa
bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.
Aidha katika Mkutano vijana hao kutoka vyama
vya CHADEMA, CUF, NCCR – Mageuzi na CHAUMA waliingia kwenye mkutano huo
kwa kile walichoashiria kuwa ni majonzi waliyokuwa nayo juu ya muswada huo.
“Leo hii sisi tumevaa nguo nyeusi, hatuoni ‘future’
sasa basi vijana tunataka umoja tunapinga ili tuendeleea kuwa wamoja, Taasisi
zote za vijana nchi hii kwa mara ya kwanza tutatangaza safari na tutauchana
muswada ukiwa unataka kuingia bungeni,”
amesema Likapo Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT wazalendo.
“Muswada unampa mamlaka msajili kutoka kuwa mlezi wa
vyama vya siasa, hadi kuwa mdhibiti wa vyama vya siasa, hivyo basi baada
ya kuutafakari kwa kina muswada huu, tumeona ndoto za vijana ziko hatarini kufa
kabisa na hali ya vijana itakuwa mbaya zaidi kuliko hata ilivyo sasa,
hatukubaliani nao hata kidogo,” amesema Patric Ole
Sosopi, Mwenyekiti
BAVICHA.
Aidha Mwenyekiti wa JUVI-CUF taifa ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Hamidu Jabali, amesema kuwa
mchakato wa vikao vya upembuzi wa muswada huo vinaendelea baada ya kila chama
kutoa wajumbe wanne watakoingia katika timu waliyoiita ya ufundi ambapo watatoa
tamko rasmi baada ya kumaliza mchakato huo.
Post a Comment