Waziri Wa Kilimo Atangaza Kiama Kwa Wasambazaji Wa Mbegu Feki
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, 24 Novemba 2018 ametangaza kiama kwa
wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku
na serikali.
Amewataka
wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo
kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha
haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale
wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.
Ametoa
agizo hilo akiwa ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine
alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI),
Taasisi iliyopewa jukumu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
la usajili wa wafanyabiashara wa mbegu (Seed Dealers).
“Serikali
imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu jambo
ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina
kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini” Alikaririwa Mhe Hasunga
Waziri
huyo pia ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI)
kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka maagizo
ya serikali pamoja na taratibu na sheria za nchi.
“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu mbegu feki jambo hili serikali haiwezi kukubaliana nalo hivyo TOSCI wanapaswa kusimamia kwa weledi ukaguzi na usajili wa Mbegu bora, pia ni lazima kuwabaini wasambazaji feki wa mbegu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema
Wizara ya Kilimo imepewa jukumu mahususi la kuhakikisha sekta ya kilimo
inaimarika kwa usimamizi madhubuti wa sera, kanuni, taratibu na
miongozo mbalimbali hivyo kunapokuwa na kelele za wananchi kuhusu mbegu
feki ni dhahiri kuwa Taasisi zenye jukumu hilo hazitekelezi kazi yake
kwa weledi.
Mhe
Hasunga alieleza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaongeza
thamani ya mazao yote yanayozalishwa nchini, sambamba na kutafuta masoko
mazuri.
Vilevile, ameitaja Wizara ya Kilimo kuwa ina wataalamu wengi hivyo unaandaliwa mfumo mzuri wa kuwaunganisha watalaamu hao ili kujadili kwa pamoja namna ambavyo kilimo kinaweza kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara ili kutoa malighafi za kutosha zitakazohuisha serikali ya viwanda.

Post a Comment