UPELELEZI KESI YA ZITTO KABWE WAIVA
Upelelezi wa kesi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, umekamilika.
Hayo
yamebainika leo Jumatatu Novemba 26, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu ambapo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Kesi ya Zitto iko mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi na imepangwa usikilizwaji wa awali Desemba 13 mwaka huu.
Inadaiwa
Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo mshtakiwa akiwa katika
mkutano huo kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya
Jeshi la polisi alitoa Maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na
chuki.
Katika
shtaka la pili, Kweka alidai kuwa siku na mahali hapo, Zitto
Kijitonyama alitoa Maneno ya uchochezi ambayo yalikuwa na lengo lenye
kuleta hofu.
Aidha Zitto anadaiwa Kutoa waraka kwa umma ukiwa na Maneno ya kichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya polisi.
Post a Comment