HUU NI MRADI WA TOFAUTI JIJINI DAR ES SALAAM.
Mwambawahabari
Hayo yamesemwa leo na mgeni rasmi kaimu Mkuu wa Wilaya ambaye pia ni Afisa tawala wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ubungo bi. Diana Kalumuna Nkarage wakati wa kuzindua mradi wa kuchakata maji taka katika kata ya Mburahati uliodhaminiwa na wizara ya mazingira ya Ujerumani kupitia taasisi ya hali ya hewa ya kimataifa kupitia mradi wa Borda-Tanzania.
Mgeni rasmi aliwashukuru wahusika wa mradi wa *BORDA* kwa kudhamini mradi huo na kuwathamini wananchi wa Mburahati. Si hilo tuu lakini pia aliwaomba wananchi kuupokea mradi na kuutumia vizuri.
*Hapa tulipo tupo kwenye mradi lakini hakuna harufu hata kidogo tuna hewa safi kabisaa.* Aliongeza mgeni rasmi. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mradi huu una umuhimu kwetu na kwa afya zetuu.
Nimtake mh. Diwani na watendaji kuanzia ngazi ya Manispaa hadi mitaa kuhakikisha wanaulinda na kuuhudumia mradi huu kwa manufaa ya wananchi wa Mburahati na Manispaa ya Ubungo kwa ujumla.
Naye mwakilishi wa *BORDA - TANZANIA* bi. Joyce Zablon Musira, alisema mradi umekuja sababu kubwa ikiwa ni kulinda mazingira ili yawe safi na salama, lakini pia utakuwa na manufaa kwa wananchi kwani utapunguza gharama za unyonyaji maji taka.
Vile vile mradi huo una msaada mkubwa kwani unaweza kutoa gesi asilia inayoweza kutumika kwa matumizi ya nyumbani.
Aliushukuru uongozi wa Manispaa na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano waliouonyesha tangu kuanza kwa mradi.
Mh. diwani wa kata ya Mburahati, Yusuph Omary Yenga kwa niaba ya wananchi aliwashukuru Borda-Tanzania kwa kuwaona kwa jicho la pili na hatimaye kuwaletea mradi huo wa kuchakata maji taka.
Aliushukuru pia uongozi wa Manispaa na Mhandisi wa maji eng. Ramadhani Mabula kwa kuwa bega kwa bega na mradi huo hadi umefikia hatua ya kuzinduliwa.
*IMETOLEWA NA*
*OFISI YA HABARI NA UHUSIANO*
*MANISPAA YA UBUNGO*
Post a Comment