WATOTO 32,000 KUPATIWA DAWA ZA MINYOO,KICHOCHO KIGAMBONI
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kupatiwa dawa hizo kwa ajili ya magonjwa ya minyoo ya tumbo na Kichocho.
Mh.Msafiri ameyasema hayo katika semina ya kuwajengea uwezo wataalam ya Idara ya Afya katika Manispaa ya Kigamboni iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya kata ya Mji Mwema- Kigamboni.
''kumekuwa na dhana potopfu juu ya hizi dawa zinazogarimiwa na serikali kwa baadhi ya wazazi kuwazuia watoto wao kumeza dawa kwa visingizio visivyo na maana kabisa" aliongeza Mh. Msafiri.
Kwa upnde wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.David Sukali amesema ofisi yake imeshafanya maandalizi yote ikiwa na pamoja na kupeleka hela katika shule zote za msingi za serikali na binafsi zitakazoshiriki katika zoezi hilo hivyo hakutakuwa na sababu ya watoto walengwa kutopatiwa dawa kama ilivyokusudiwa siku hiyo ya tarehe 03/09/2018.
Naye Mganga mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dr. Charles Mkombachepa amesema ili mtoto apewe dawa ni lazima awe amepata uji ndiyo maana serikali imegharimia na kuhakikisha kila mtoto anapata uji kabla ya kumeza dawa. Dr.
Mkombachepa ameongeza kuwa ofisi yake imetoa semina kwa walimu kutoka katika shule zote 45 zitakazoshiriki katika zoezi la utoaji dawa.
Kuhusu walengwa wa zoezi hili , Dr. Mkombachepa amesema ni watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka 5 waliopo katika shule ambapo katika awamu hii zaidi ya wanafunzi 32,000 walipo katika mfumo rasmi wa shule za msingi watapatiwa dawa.
Akifunga semina hiyo, Mkuu wa Wilaya Kigamboni Mh.Sara Msafiri amesema kwamba zoezi hilo limepangwa kufanyika siku moja ya tarehe 03/09/2018 lakini ametoa wito kwa wazazi wale ambao watoto wao hawatapata dawa siku hiyo wafike katika zahanati na vituo vya Afya vyote ndani ya Kigamboni ili kupata dawa hizo ambazo zinatolewa bure bila malipo yoyote.
Post a Comment