Ads

NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA

Mwambawahabari


Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma


IKIWA msimu wa kununua mazao

umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula

(NFRA), Vumilia  Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia

ubora wa mahindi.


Aidha, amesema nchi inachakula

cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei

ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.Akizungumza na waandishi wa

habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua
mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo
yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.



" Haiwezekani NFRA itumia

fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu

kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia

viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..


Aliongeza: “Lazima chakula

tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe taswira ya NFRA kwa sababu

awali kulikuwa na tatizo la chakula kuharibika kwa kipindi kifupi.”



Zikankuba alisema ili

kuhakikisha mahindi ya wakulima yanaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa NFRA

tayari imekwishatoa elimu kwa wakulima kupitia vikundi na kwenye vyombo vya

habari.Alibainisha kuwa baada ya elimu
hiyo wakala umefanikiwa ambapo wakulima kutoka maeneo ya Makambako, Sumbawanga na
Mpanda wameanza kuzalisha na kuuza mahindi yenye ubora kwa NFRA.



“Changamoto iliyopo ni kwa

baadhi ya wakulima wachache ambao bado wamekuwa wagumu kubadilika na wale ambao

wanaamini wakitumia nafasi zao wanaweza kuuza mahindi yasiyo na ubora,"Alisema kwa mkulima kuwa na

mahindi yenye ubora unatoakiwa utasaidia katika kupata soko la NFRA, pia katika
taasisi zingine zinazonunua nafaka hiyo za ndani na nje ya nchi.



Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba.

No comments